Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, September 14, 2023

KUMBUKIZI YA TUNU ZA AFRIKA TULIZOJALIWA NA MWENYEZI MUNGU.




 wake wa Marais hao, Mama Maria Nyerere mwenye gauni nyeupe na aliyekuwa mke wa Mandera Mama Mandela au Mama Masheri, Mwenye gauni la kitenge


Na Dustan Shekidele,Morogoro. 

VIONGOZI waadilifu barani Afrika Rais Mstaafu wa awamu ya kwanza Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere’Baba wa Taifa’[kulia]akiwa na swahiba wake mkubwa Rais Mstaafu ‘Mzalendo’ wa  Afrika Kusini hayati Nelson Mandela.

Mwalimu Nyerere alipofariki dunia nchini Uingereza 0ctobar 14- 1999, aliyekuwa Marikia wa nchini hiyo aliutangazia  ulimwengu juu ya kifo hicho alisema.

” Bara la Afrika kulikuwana taa mbili zinazoangazia bara hilo na Ulimwengu mzima Julius Nyerere na Nelson Mandela.

Leo taa moja imezimika Nyerere amefariki dunia hapa Uingereza hivyo imebaki taa moja Nelson Mandera”

Enzi za uhai wa Marais hao hawakuwa na uroho wa madaraka kama baadhi ya marais wengine,wao waliong’atuka madarakani kwa hiyari yao ili hali bado wakipendwa na Wananchi wao.

Marais hao wakiwa madarakani na baada ya kung’atuka  walijitosa kupatanisha mataifa ya Afrika yaliyokuwa na Migogoro ya kiuongozi na Vita vya wenyewe kwa wenyewe sambamba na kuzisaidi nchi sisizokuwa Uhuru kupata Uhuru.

Kwenye utawara wao, Nyerere na Mandela wameacha misingi mizuri kwenye mataifa yao inayoendelea kutawara Mpaka sasa.

Tanzania Nyerere aliondoa Ukabira na Udini kuondoa tofauti kubwa ya walionacho na wasio nacho.

Kwa Upande wake Mandela aliyefariki dunia Desemba 6- 2013 aliondoa ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini kati ya Wazungu na Waafrika ambapo alikubari kutoa sehemu kubwa ya Maisha yake akikubari kufungwa Magereza miaka 27 akishikilia msimamo wake wa kupinga Siasa za ubaguzi wa rangi zilizolewa na Makaburu.

Mungu wabariki Viongozi wetu hawa huko waliko na awasamehe makosa yao machache na uwape Pepo kwa mema yao mengi.

“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe wote tuseme Amen.”

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...