Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, September 17, 2023

BODA BODA ATAPELIWA PIKIPIKI KIAINA

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa juu ya Pikipiki yake ya Mwendokasi.

 

.JUMBE WA NENO LA MUNGU.

YAREMIA 33.3

“ Niite  name nitakuitika,namI nitakuonyesha  mambo makubwa magumu usiyoyajua.”

“Call unto Me  and l will answer thee.and shew  thee great and Mighty things which thou knowest not” Hilo ndilo neno letu la Leo Jumapili ya Septemba 17.

       UCHAMBUZI WA NENO HILO.

Baadhi ya watu hapa duniani wakipata changamoto baada ya kukimbilia kwa Mungu wanakimbilia kwa Waganga wa Kienyeji ’binadamu wenzao’.

Ndugu zangu hao Wanganga hawatawasaidia kitu zaidi ya kukuongezea tatizo.

 Nimeradhimika kuandika ujumbe huo baada ya tukio lililotokea wiki iliyopita.

Kunarafiki yangu Mmoja jina nalihifadhi  boda boda yake imeibiwa maeneo ya Mikese.

MAZINGIRA YA KUIBIKWA PIKIPIKI HIYO.

Rafiki yangu huyo baada ya kununua Piki piki hiyo kamkabidhi kijana amretee kipanda kila siku elfu 10.

Unajua tena mambo ya kijijini baada ya watu kuiona Chombo hiyo Mpya inaendeshwa na kijana mdogo, Matapeli wameingia kazini na kumtapeli kisomi.

Akinielezea A-Z mazingira ya tukio hilo rafiki yangu huyo alifunguka haya.

” Kijana wangu anadai kuna mtu alimkodisha akiomba ampeleka kituo cha Polisi akamshitaki  jirani yake aliyempiga Mwanae.

Walipofika Polisi jamaa kaingia ndani na kazuga zuka huku kijana wangu akiwa nje na Pikipiki baada ya dakika kama 10 hivi tapeli huyo aliyekuwa ameficha karatasi mfukoni alivyotoka nje kazichomoa  karatasi na kuzishika mkononi.

Akamwambia boda boda wangu ampele Pikipiki akatoe Photo Copy kwa vile ni mazingira salama ya Polisi Kijana wangu hakuwa na wasi wasi kamkabidhi funguo tapeli huyo aliyetoweka na Pikipiki yangu jumla.

 Tumeitafuta leo siku ya tano hatukuipata hivyo nataka kuhamia upande wa pili niende kwa wataalamu’Waganga wa Kienyeji kuangalia labda watanisaidia kuipata”alisema jamaa huyo.

Mwandishi wa Mtandao huu alipingana vikali na jamaa huyo na kuamua kumshauri  asifanye hivyo badala yake akazungumze na wazazi wa kijana huyo wangalie namna ya kumlipa deani hilo la Pikipiki.

Nashukuru rafiki yangu huyo amepokea ushauri wangu ambapo baada ya kikao kufanyika wazazi  wamekubali kulipa deni hilo kwa kumkatia heka moja ya Shamba na shwala hilo limeisha hivyo na rafiki yangu huyo amerudia kwangu na kunipa asante kwa ushauri mzuri niliompa.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...