Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, September 3, 2023

KIPIMO MPIMACHO NDICHO KILE KILE MTAKACHOPIMIWA.





 

 

                     LUKA 6.38

“Wapeni watu  Vitu,nanyi mtapewa,kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa sukwa hata kumwagika,ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu.

Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho  mtakachopimiwa.”

“Give and it Shall be given unto you,good measure,Pressed down and shaken  together, and running Over,Shall men give into your bosom.

For with the same measure that ye mete withal it Shall be measured to you again.” Hilo neno letu la leo Jumapili ya Septemba 3.                    UCHAMBUZI.

Kipimo kile kile unachompimia mwenzio ndio hicho hicho Mungu naye atakachokupimia. Ukimfanyia mwenzio ubaya  wa aina yoyote  Mungu atakulipa kwa kipimo kile kile ulichomfanyia mwenzio hapa hapa duniani .

Halikadharika Kipimo cha wema ulichompimia mwenzio  Mungu naye atakulipa kipimo kile kile hapa hapa duniani.

Mwenyemasikio na alisikie agizo hili la Mwenyezi MUNGU  Muumba wa Mbingu na Ardhi,

Asiyefananishwa na kulinganishwa na kitu Chochote Duniani na Mbinguni.

Picha mbali mbali mtumishi wa Mungu Dunstan Shekidele akiwapa Msaada watu wenye uhitaji.

Hakuna mtu aliyefirisika hapa chini ya Jua kwa kuwasaidia watu wenye uhitaji au kutoka Sadaka Kanisani na Msikitini, kumcha Mungu ni Chanzo cha Maarifa.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...