Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, September 2, 2023

BAADA YA MAWENZI MARKET KUPIGWA BEI, WADAU MORO WAMEINUNUA TIMU YA FOUNTAIN GATE.

Godfrey Kombani mwenye kaptura nyeupe na jezi ya Mawenzi Market akiwa na Mwandishi wa habari hizi[[Kulia’

God Kombani akiwa na Mdau wa Soka Mkoa wa Morogoro Msanii Mkongwe wa Muziki wa kizazi Kipya Seleman Msindi’Afande
 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
BAADA ya Uongozi wa timu ya Mawenzi Market kuipiga bei timu hiyo kwa Mwanasiasa maarufu mkoni Singida, Wadao wa soka mkoani Morogoro wakiongozwa na Jerry Junior wamefanikiwa kuinunua timu ya Fountain Gate ya Mkoani Dodoma. 
 
Miaka 3 iliyopita Uongozi wa timu ya Mawenzi Market iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza’ChampionShip’kukumbwa na ukata wa kifedha waliamua kuikabidhi timu hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ambaye hukuweza kuipokea. 
 
Kufuatia hali hiyo Viongozi wa timu hiyo inayomilikiwa na wafanyabiashara wa Soko la Matunza la Mawenzi kwa kauli moja walikubalia kuipiga bei. 
 
Kwa sasa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ‘Mwanamichezo’ Adamu Kigoma Malima mkoa wa Morogoro kupitia kwa wadau wa Soka wamefanikiwa kuinunua timu ya Fountain Gate inayoshiriki ligi daraja la kwanza’ChampionShip’. 
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa Umma na Uongozi wa Fountain Gate baada ya biashara hiyo kukamilika rasmi timu hiyo imebadilisha jina ikiitwa FGA Talents. 
 
lfahamike Uongozi wa Fountain Gate umeamua kuipiga bei timu hiyo baada ya wao kununua hisa kwenye timu ya ligi kuu Singida Big Stars ambapo baada ya makubaliano hayo kwa sasa timu hiyo imebadili jina ikiitwa Singida Fountain Gate.
 
Ligi daraja la kwanza imepangwa kuanza Jumamosi ijayo huku timu ya WanaMorogoro FGA Talents, itaanza mbio zake za kupanda ligi kuu ikiutumia Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwenye michezo yake yote. 
 
Wadau wa Mkoa wa Morogoro Mnaombwa kunganisha nguvu kuhakikisha timu hiyo inapanda ligi kuu msimu ujao. 
 
Awari Mawenzi kabla ya kukumbwa na Ukata mkali wa kifedha ilikuwa ikifadhiriwa na Godfrey Kombani’ Mtoto wa Waziri wa awamu ya 5 Marehemu Celina Kombani Mbunge wa Jimbo la Mahenge Mkoani Morogoro.
.
 

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...