Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, September 18, 2023

MTETEZI WAWNYONGE MH ABOOD AKISIKILIZA SHIDA YA BIBI


 

KUMBUKIZI.

 Kweli Mh Dr  Aziz Abood ni Mtetezi wawanyonge alistahiri kupewa tuzo ya Udaktari na .moja ya Vyuo Vikuu vya nchini Marekani.

 Moyo wa kuwasaidia watu na kuwatetea   wangonge hakuanza jana wala juzi, picha hii nilipiga Julai 2015 utawara wa awamu ya Nne ambapo Mh Abood aliamua kuzunguka Mitaani kwa miguu akisikiliza changamoto za wananchi.

Alipofika eneo la Lunna alikutana na bibi huyo ambaye alimsimamisha Mh Abood ambaye kwa unyenyekevu mkubwa alimsogelea bibi huyo kama anavyoonekana Pichana na kumuliza Changamoto zinazomkabiri.

Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa jirana na tukio hilo alimsikia bibi huyo akimueleza Mh Abood kwamba Changamoto yake hana pesa ya kununua futari ikumbukwe mwezi huo ulikuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

 Bila hiyana Mtetezi huyo wawanyonge alizama  mfukuni katoa kiasi cha pesa na kumkabidhi bibi huyo ambaye mara baada ya kupokea kiasi hicho cha Pesa alimuombea madua wote mazuri Mh Abood likiwemo dua la kumuombea Maisha marefu.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...