Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, August 31, 2023

AMINA KIANDO AZIDI KUPIGA MWINGI.

                                       Amina Kiando

 ...Amina Kiando akiongoza timu za Mtibwa na Mbeya City kuingia uwanjani, kulia ni mkufunzi wake Refa Martin Saanya

 

             Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Mwamuzi Chipukizi wa kike  Amina Kiando Mkazi wa Mkoani Morogoro anazidi kupiga mwingi kwenye kazi yake ya Uamuzi wa mpira wa Miguu.

lkumbukwe mwaka 2017 Mtandao Pendwa wa Shekidele uliriripoti Makaka iliyomhusu refa huyo, baada ya Mmoja wa wakufunzi wake, Afande Martin Saanya Pichani [kulia mwenye beji ya FIFA kumpa nafasi ya kuchezesha mchezo mkubwa uliozikutanisha timu kubwa za ligi kuu Mtibwa Sugar na Mbeya City.

Licha ya kuwa madaraja ya chini wakati huo lakini aliaminiwa  na kupangwa kuchezesha mchezo huo mkubwa.

Gemu hiyo  Maalumu ilidhaminiwa na kanisa  la Baptist ulipigwa Julai 29 2017 kwenye tamasha la kanisa hilo lililofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Kwenye mchezo huo Amina Kiando alichezesha vizuri hali liliyopelekea Mwandishi wa habari hizi kuvutiwa na uwezo wake na kumwandikia makalla hiyo iliyomtabilia kufika mbali kwenye kazi yake hiyo ya refa.

Hatimaye  refa Amina  ameanza kufika mbali baada ya sasa kupanda daraja na kuteuliza kuchezesha michezo migumu ya Ligi kuu Tanzania Bara.

Miongoni mwa michezo hiyo ni mchezo wa juzikati wa nusu fainali ya mchuano ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Singida Big Star uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na Simba kuibuka na ushindi.

Mtandao huu unazidi kumshauri Amina asibweteke na mafanikio hayo bali aendelee kupambana hadi kufikia hatua ya kuvishwa beji ya FiFA na kuchezesha michuano mikubwa barani Afrikani.

Hakuna lisilowezekana hapa chini ya jua kama utafanya kazi yako kwa kutenda haki na kusimamia amri za mwenyezi Mungu na sheria za nchini na sharia 17 za mchezo huo wa Soka.

 Vile vile Mtandao huu unasema ni kosa kubwa kukata tamaa kwa jambo ambalo hujui mwisho wake utakuaje.

Wao waweze wanani? wewe ushindwe unanini?

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...