....Akiwa Mbuga ya Mikumi akitokea Kilombero
....Akiwa Dumila
.....Akiwa Kilosa Mjini
....Akiwa eneo la Bwawani akitokea Chalinze
.....Akiwa katikati ya Msitu akitokea Matombo Wilaya ya Morogoro Vijijini
....Akiwa juu ya Mlima wa Ng'alo akitokea Kinole Morogoro Vijijini
.......Hapa akiziba pacha saa 4 usiku eneo la Turiani akitokea Kilindi Mpakani mwa mikoa wa Morogoro na Tanga
.......Akiwa hosipital ya Kijiji cha Berega
Padri akiimwagia maji ya baraka Pikipiki ya Mwandishi wa Mtandao huu akidhamini kazi ngumu anayofanya Mwandishi huyo
ZABURI 40.1-5
“Nilimgoja Bwana kwa saburi akaniinamia akakisikia kilio changu.
Akanipandisha toka shimo la uharibifu toka udongo na Utelezi,akaisimamisha miguu yangu Mwambani, akiziimarisha hatua zangu.
Akatia Wimbo mpya kinywani Mwangu,ndio sifa zake Mungu wetu wengi wataona na kuogopa, nao watamtumaini Bwana.
Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake,wala hakuwaelekea wenye kiburi,wala hao wanaogeukia Uongo.
Ee Bwana Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na Mawazo yako kwetu, hakuna awezaye kufananishwa nawe, kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri,nimengi sana hayahesabiki”.Hilo ndilo neno la leo Jumapili ya Agosti
UCHAMBUZI,
Namshukuru Mungu anazidi kunisimamia katika hatua zangu ndefu za Safari za Vijijini kwa kutumia usafiri wa Pikipiki napita sehemu hatarishi zenye wanyama wakali Kama vile Simba,Chui na Tembo.
Napita kwenye mabonde,Milima na Misitu Mineno, nyakati zote za usiku na mchana nikitoa sadaka maisha yangu kuwatumia watu wengi wenye uhitaji.
Mara nyingine napata Pacha katikati ya Mistu Mnene nyakati za usiku nalazimika kukokota Pikipiki hadi kijijini na kuziba Pacha usiku huo mnene kwa kutimia tochi ya Simu kama inavyoonekana Pichani.
Ama kwa hakika kazi hii inahitaji wito wa dhati kutoka ndani ya Moyo,nashukuru Mungu changamoto hizi kamwe hazijawahi kunikatisha tamaa ya kuwatumika wenye uhita.
Kwa kutambua kazi ngumu anayofanya Mwandishi wa Mtandao huu kiongozi mmoja wa dini aliamua kuimwagia maji ya Baraka Pikipiki ya Mwanahabari huyo.
Nawasihi Walimwengu na kuisihi nafasi yangu sisi wenye nafasi tujitoe kwa kutumia nafasi zetu au mamlaka zetu kuwasaidia watu wenye changamoto mbali mbali.
Yesu Kristo [Nabii lssa]aliamua kutoa Maisha yake binafsi kwa kusurubiwa kwa kupigwa mijeredi, kisha kutundikwa msalabani na kuviswa taji la Miba kwa lengo la kutukomboa sisi wanadamu na kupitia Mateso yake hayo sisi tumepona mpaka hii leo.
Mwenye Masikio na asikie.
No comments:
Post a Comment