Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, August 18, 2023

BLACK VIBA MABINGWA MICHUANO YA NDONDO CUP.

Beki wa timu ya Black Viba Feisal Yassin akifanya vitu yake ya kujiamini kama beki  mpya wa Simba Mcameroon’MVP’ Chamalon.





Kipa wa Black Viba Mfaume Gumbo akijiandaa kunyaka Mpira huku akiasama mdomo kama chatu anayetaka kummenza Mbwa.

lkumbukwe Kipa huyo hadi timu ya Gwambina Fc ya Mkoani Mwanza inavunjwa na Mmiliki wa timu hiyo kwa sababu za kiutawala Kipa huyu alikuwa kipa namba moja wa timu hiyo.

Baada ya  kuvunja Gumbo ameamua kureja nyumbani kwake Vibandani Kata ya Mbuyuni Mkoani Morogoro.


Afisa habari wa Black Viba’Dogo Menti aliyekuwa akizunguka uwanja Mzima akihamasisha Vijana wake kusaka ushindi, akinyoosha Mikono juu kulalamikia mchezaji wake kuangushwa chini.


 


Refa alipuliza Kipenga na beki Kwasi akipiga faulo hiyo.
Dogo Menti akiwa kwenye Benchi la timu yake akiendelea kuhamasisha

         Feisal akiruka juu na kuondoa hatari langoni mwake
 


 Na Dustan Shekidele,Morogoro.

WATOTO wa Kishua kutoka Mitaa ya Vibandani jirani na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ‘SUA’Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro Black Viba’Chama la Wajanja’ jana jioni wametwaa ubingwa wa Michuano ya Kilakala Ndondo Cup.

Vijana hao wanaoongozwa na Diwani wa Kata ya Mbuyuni Mh Samwel Msuya walitwaa ubingwa huo wa kungombea Mnyama Ng’ombe baada ya kuifunga timu ngumu ya Kichangani United Kutoka Kata ya Kichangani bao 1-0.

Fainali hiyo iliyokuwa kali kwa muda wote wa dakika 90 ilipigwa jana uwanja wa CCM Saba saba na washindi walijipatia bao hilo pekee kipindi cha pili.

Akizungumza na Mtandao huu Mratibu wa Michuano hiyo  Nicodemas Msike alisema awari michuano hiyo ilikuwa kichezwa uwanja wa wazi wa Kilakala Makaburini na kwamba ilipofikia hatua ya fainali waliamua kuihamishia  uwanja huo wa Saba saba na mashabiki walilipa elfu moja getini.                     

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...