Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, August 21, 2023

HII KALI,BAADA YA MANISPAA YA MORO KUKOSA TIMU YA LIGI KUU MFANYABIASHARA AFUNGUA OFISI MAKABURINI.

 
Mmachinga Clemence Josephe akiuza Maji Makaburini wakati watu wakiendelea kuzika


            ......Akiuza Maji Uwanja wa Saba saba kwenye
 


              Na Dustan Shekidele,Morogoro.

KUFUATIA Wilaya ya Morogoro Mjini kukosa timu ya Ligi kuu, Ligi daraja la kwanza na Ligi daraja la Pili Mfanyabiashara ndogondogo’Machinga’ Clemensi Joseph amejiongeza na kuamua kufanyabiashara yake ya kuuza Maji Makaburini.

 Awari wakati Manispaa ya Morogoro ikimiliki timu 4 kwenye madaraja wote matatu, Polisi Morogoro’Wana Ngunguri’ iliyoshiriki Ligi Kuu, Mawenzi Market’Jogoo la Mji’ na Burkinafazo’Wanakisiki cha Mpingo’ zilizokuwa Ligi daraja la Kwanza na Saba saba United iliyoshiriki daraja la Pili.

Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia Joseph akifanyabiashara hiyo ya Maji Uwanja wa Jamhuri wakati timu hizo 4 zikishiriki michuano hiyo.

Miaka ya hivi karibuni timu hizo zilitoweka Manispaa ya Morogoro kwa sababu mbali mbali, Polisi Morogoro ilihamishiwa Mkoa wa Kilimanjaro na kubadirishwa jina ikiitwa Polisi Tanzania.

 Mawenzi Market baada ya kukumbwa na ukata wa Pesa Viongozi wa timu hiyo waliamua kuipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wa wakati huo akiwa Loata Ole Sanare ambaye hakuweza kuipokea, ili timu isiwafia kwa kushishushwa madaraja na TFF Kwa kushinda kufika kwenye kituo cha Mchezo.

Viongozi watimu hiyo kwa kushirikiana na wanachama wao kwa kauli moja walikubaliana kuipiga bei timu hiyo kwa Mwanasiasa Mmoja kutoka Mkoa wa Singida, huku Burknafasa na Saba saba United zikishuka madaraja hadi daraja la tatu baada ya kukumbwa pia na ukata wa Pesa.

Kufuatia hali hiyo ya Manispaa ya Morogoro kukosa timu kwenye madaraja hayo, kumewaadhiri watu wengi wakiwemo wafanyabiashara.

Wiki iliyopita Mwandishi wa habari hizi alitinga  Makaburi ya Kolla Manispaa ya Morogoro,kushiriki Mazishi ya Marehemu Sorome Mdede tuliyemzika Agosti 8 na Catherine Mapunda tuliyemzika Agost 9.

 Kwenye Mzishi hayo Mtandao Pendwa wa Shekidele  ulimshuhudia Joseph akiwa na Lundo la katoni za Maji akizunguka eneo lote la Makaburi hayo yaliyogawanywa sehemu pili za Wakristo na Waislamu akiwauzia maji waombolezaji waliofika makaburni hapo kuwapunzisha wapendwa wao.

Akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi Joseph Maarufu ‘Seneta Mzee wa Masika’alisema.

 “Shekidele kama unavyojua biashara yangu ya maji nauza Uwanja wa Jamhuri na Saba saba kwenye michezo ya ligi, kuu, Ligi daraja la kwanza na Ligi daraja la Pili, Kwa sasa  timu zote za Manispaa zimeuzwa nyingine zimeshuka daraja ili nisife njaa nimejiongeza biashara yangu ya Maji kwa sasa naifanya hapa Makaburini namshukuru Mungu hapa biashara ni nzuri”alisema Mmachinga huyo.

Kwa sasa Mkoa wa Morogoro unaongozwa na Mkuu wa Mkoa  Adam  Malima ambaye ni Mtu wa Mpira, na taarifa za awari zinadai chini ya Uongozi wake wa Muda Mfupi mkoani hapa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho ya kuinunua timu ya Fountain Gate ya Dodoma inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...