Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, August 6, 2023

WATOTO WA MKURUGENZI WA KATIBA NCHINI WABEBA JUKUMU LA KUSOMA SOMO LA KWANZA NA WASIFU WA BABA YAO

                             Miachael akisoma somo la kwanza
Naibu waziri na kigogo wengine wa Wizara ya Katiba na Sheria

                             Marehemu Luanda enzi za Uhai wake
Mjane wa Marehemukulia] na wanane wakinyoonyasha mikono juu ikiwa ni kiashilia cha kupokea Sakrameti takatifu

 Lydia Luanda Mjane wa Marehemu akila na kunywa mwili na damu ya Yesu Kristo'Sakramenti Takatifu'

.
                                       Na Dustana Shekidele,Morogoro.
WATOTO wa Watatu wa Mkurugenzi wa Katiba, Ufuatiliaji Haki, hayati Kharist Michael Luanda, wamebeba jukumu la kuongoza ibada kwa kusoma somo la Kwanza pamoja na Wasifu wa Mpendwa baba yao. 
 
Mara baada ya lbada ya kumuombea Mpendwa baba yao iliyoongozwa na Paroko wa Parokia ya Tawa Padre Leande Jaka kuanza, Michael ambaye ni mtoto wa Pili wa marehemu aliamua kusoma somo la kwanza kwenye lbada hiyo iliyofanyika nje ya nyumba yao. 
 
Kama hiyo haitoshi ilipofika wakati wa kusoma wasifu wa Marehemu, Birtrice ambaye ni mtoto wa kwanza wa Marehemu aliwakusanya wadogo zake Michael na Banni na kusoma Wasifu huo wa Mpendwa baba yao. 
 
                                          WASIFU.
“Marehemu alizaliwa hapa kijijini Lukenge Kata ya Kibungo Juu Tarafa ya Matombo Morogoro Vijijini June 19.1966.
 
Alisoma shule ya Msingi Lukenge iliyopo hapa hapa kijjiji alihitimu darasa la saba 1982 na kufanikiwa kwenda sokondari Mkoa wa Pwani.
 
Alihitimu kidato na 6 na kujiunga na Jeshi la kujenga taifa kwa mujibu wa sheria, baadae alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea sheria ambapo alihitimu chuoni hapo Mwaka 1993. 
 
Alipata ajira Serikalini akiwa mwanasheria wa halmashauri ya Jiji la Mbeya,kabla ya kupanda cheo na kuwa Wakili wa Serikali baadae akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Katiba, Ufuatiliaji Haki cheo alichohudumu hadi Umauti unamkuta Julai 27 kwenye hosipital ya Mloganzira Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabi ya ugonjwa wa shinikizo la damu’Presha’.
 
Marehemu ameacha Mjane na watoto watatu, Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimiziwe.
 
Padre Jaka amtaja Hayati Makufuli akimsifu Marehemu Luanda, habari hiyo itaruka hewani hivi Punde

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...