Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, August 5, 2023

JAJI MSOFE AWAFARIJI WATOTO WA MKURUGENZI WA KATIBA HAYATI LUANDA.

Mh Jaji Msofe akizungumza maneno hayo ya hekima.
 


                Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MWENYEKITI wa Tume ya kurekebisha Sheria nchini, Jaji Mstaafu January Msofe ameifariji familia ya Mkurugenzi wa Katiba Ufuatiliaji Haki, Marehemu Kharist Michael Luanda.

Jaji Msofe kabla ya kutoa salamu zake za Rambi rambi aliifariji familia hiyo hususani watoto watatu wa Marehemu, Bitrice, Michael na Benni akiwapa maneno ya faraja yaliyowatia nguvu kipindi hiki kigumu walichompoteza Mpendwa baba yao huku wakiwa bado wadogo wakihitaji zaidi malezi na Muongozo wa Mzazi wao huyo.

”Sisi tulimpenda Luanda lakini Mungu amempenda zaidi niwatie nguvu watoto wa marehemu, ili limeshatokea jipeni nguvu muendelea na Maisha, mimi baba yangu alifariki dunia nikiwa na umri wa miaka 8 uona sasa naendelea kuishi mpaka kufika umri huu wa Uzee”alisema Jaji Msofe.

Baada ya maneno hayo ya faraja Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa bize kukusanya matukio Msibani hapo aliwaangalia watoto hao na kuwashuhudia  wakina na nyuso za faraja baada ya kusikia maneno hayo ya hekima kutoka na Kigogo huyo wa sheria nchini.

Baadae watoto hao wa Marehemu wote watatu walibeba jukumu la kusoma wasifu wa Mpendwa baba yao, tukio hilo litaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...