Wananchi wa Kijiji cha Lukenge wakimsikiliza kwa makini Padrre Jaka.
Marehemu Luanda enzi za Uhai wake
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
PADRE Leande Jaka ametoa ushauri kwa Rais wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli’JPM.’aliyekuwa na kauli mbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’ Kwenye utawara wake
Kiongozi huyo wa dini alitoa ushauri huo alipoongoza lbada ya kumuombea Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki, Marehemu Kharist Michael Luanda aliyefariki dunia Julai 27 na kuzikwa kijijini kwake Lukenge Matombo Morogoro Vijijini Julai 31.
”Ndugu zangu hapa duniani tunapita hivyo tunapofanya kazi tukumbuke sala na swala, nakumbuka utawara wa hayati Magufuli kwenye kauli mbiu yake alisema Hapa Kazi Tu, ningepata nafasi ya kuonana naye ningemshauri kwenye kauli mbiu yake hiyo aongeza maneno yanayosema Kazi na sala”alisema Padre huyo na kuongeza.
Marehemu Luanda hilo alifanikiwa licha na usomi wake na ubize wa kazi lakini alikuwa jirani na Mungu kwa kushiriki lbada mara kwa mara na kumbuka kwenye lbada ya kuuga Mwaka 2022 na kuukaribisha Mwaka 2023 alihudhuria lbada hiyo iliyofanyika kanisani kwetu hapa Lukenge.
lbada hiyo iliambatana na harambee ya kuchangia kanisa ambapo Luanda alichangia Milioni Moja”alisema Padre Jaka ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Tawa, Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro.
lfahamike Padre Jaka awari alikuwa akiongoza Parokia ya Kiwanja cha Ndege.
Maaruru Kanisa la Winga Manispaa ya Morogoro. akizungumza na Mwandishi wa habari hizi kwenye mazungumzo binafsi alisema amehamia Parokia ya Tawa miaka 2iliyopita akisimamia shule Zaidi 29 za kanisani hilo zilizpo ndani ya Jimbo lote la Morogoro.
No comments:
Post a Comment