Katibu Mkuu wa Wazira ya Katiba na Sheria Mary Makondo[kulia] akiwafariji familia hiyo
Benni Kulia akimfuta machozi dada yake, huku Michael naye akifanya hivyo kwa mama yake
Naiwabu Waziri[kati mwenye khanga nyeupe] akiangalia tukio hilo kwa uchungu mkubwa huku akitokwa na machozi, kushoto ni mwenye khanga nyekundu ni katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheri Mary Makondo na kulia mwenye koti na shati jeuoe ni Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Mh jaji Mstaafu January Msofe
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WATOTO wa wawili wa kiume wa Mkurugenzi wa Katiba, Ufuatiliaji Haki Hayati Kharist Michael Luanda, wameliza watu Msibani akiwemo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh Pauline Gelui kwa ujasili waliouonyesha kwenye Mazishi ya Mpendwa baba yao.
Mara baada ya Muongozaji’MC’ wa lbada hiyo ya Mazishi iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Kijiji Cha Lukenge Kata ya Kibungo Juu Tarafa ya Matombo, Morogoro Vijijini kuamuru familia hiyo ya Marehemu kumuaga kwa mara ya mwisho mpendwa wao.
Mjane wa Marehemu Bi,Lydia Luanda kwa uchungu mkubwa aliwakusanya watoto wake Bitrice ambaye ni wa kwanza kuzaliwa,Michael, wapili na wa mwisho Benni wakasogea kwenye jeneza lililobeba mwili wa mpendwa baba yao.
Walipofika Bitrice alikusanya mikono ya wadogo zake na ule wa Mama yake kwa pamoja wakichora alama ya Msalaba kwenye paji la Uso la Mpendwa wao.
Baada ya kufanya hivyo Mjane wa Marehemu na Mwanaye Bitrice kwa uchungu waligoma kutoka kwenye jeneza hilo wakishindwa kuamini kama kiongozi na Mlezi wao huyo wa familia amefariki dunia.
Kufuatia hali hiyo Watoto wa kiume Michael na Benni walibeba jukumu la kuwabembeza ambapo Michael alipiga magoti na kumfuta machozi Mama yake huku akimpa maneno ya faraja huku Benni akimfuta machozi dada yake kama anavyoonekana Pichani kulia.
Tukio hilo lililiza watu wetu waliokuwepo msibani hapo akiwemo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pouline Gelui[mwenye khanga nyeupe ] Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo[Wakwanza kushoto] na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu Mh January Msofe[kulia mwenye kofi na shati jeupe].
Mtandao huu unamuombe Mwenyezi Mungu azidi kuwapa nguvu na faraja familia hiyo kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mpendwa wao.
Kufuatia hali hiyo Jaji Msofe aliifajiri familia hiyo kwa kuwapa neno la faraja, habari hiyo itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment