Naibu Waziri Mh Pouline akitoa salamu za Rambirambi
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KUELEKEA Mchakato wa Katiba Mpya, Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mh Pauline Gekul amesema kifo cha Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki, Hayati Kharist Michael Luanda[57]alikuwa tegeo kubwa kwenye mchakato huo.
Naibu Waziri Pauline aliyasema hayo alipotoa Salamu za Rambi rambi kwa niaba ya Wizara kwenye Mazishi ya Marehemu Luanda yaliyofanyika Julai 31 kijijini kwake Lukenge eneo la Dabwala Kata ya Kibungo Juu Tarafa ya Matombo Wilaya ya Morogoro Vijijini.
”Kama Wizara tumepoteza mtu muhimu sana kipekee nilikuwa na mtegemea sana kaka Luanda kwenye mambo mbali mbali ikiwemo ya kujibu maswali Bunge, tulimuhitaji Kaka Luanda kuliko wakati yoyote ule kama mnavyojua tunaelekea kwenye mchakato wa Katiba, kama Wizara tukimtegemea sana kwenye mchakato huo”alisema Naibu Waziri huyo na kuongeza
Hivi karibuni nikiwa Mbeya Waziri wetu wa Katiba na Sheria Mh Dkt Damas Ndumbaro aliniambia nikutane na Kaka Luanda tuanze kujadili swala hilo la Mchakato wa Katiba”alimaliza Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini.
Baadhi ya Vigogo wengine wa Wizara hiyo walishiriki kwenye Mazishi hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msofe.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro Mh Poul Ngwembe.na Wakurugenzi mbali mbali wa Wizara hiyo.
Watoto wa Kiume wa Marehemu waliza watu Msibani Picha za tukio hilo zitaruka hewani hivi Punde, hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment