Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, August 23, 2023

TASWIRA TAJIRI ABOOD NA CLATOUS CHAMA WALIVYOUWASHA MOTO MCHEZO WA HISANI.


Manahodha wa timu za Mwamnyeto Foundation Zawad Mauya Kulia na Aziz Abood wa Moro Combine wakiwaongoza wachezaji wao kutoka vyumbani kuelekea uwaniani
Mh Abood akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Adam Malima kukagua timu ya Moro Combine


Mh Abood akisalimiana na wachezaji wa timu ya Mwamnyeto Foundation akiwemo Kibwana Shomari




Mh Abood akila mwereka baada ya koksa bao la wazi akiwa yeye na kipa wa Mohamed Nunda
Clatous Chota Chama naye akiramba nyasi za Uwanja wa Jamhuri baada ya kukwatulia ndani ya boksi
Chama akiokota mpira wavuti baada ya winga wa Mwamnyeto Foundation Offer Chikola ambaye ni winga wa timu ya Geita Gald Kupachika bao la kwanza. lfahamike Chikola ni mkazi wa Mafifa Mkoani Morogoro.





 

 

           Na Dustan Shekidele,Morogoro,

HIVI Karibuni wachezaji nyota wa Mabingwa wa Kihistoria Yanga Bakari Mwamnyeto Mwenyeji wa Tanga na Zawadi Mauya Mkazi wa Kihonda Maghorofani Mkoani Morogoro kupitia taasisi yao ya Mwamnyeto Foundation waliandaa Michezo 2 ya hisani ya kuchangia watu wenye uhitaji.

Mchezo wa kwanza ulipigwa Julai 3 Uwanja wa Mkwakwani Tanga nyumbani kwa Mwamnyeto na mchezo wa Pili ulipigwa Julai 7 Uwanja wa Jamhuri Morogoro nyumbani kwa Zawadi Mauya .

Katika gemu hiyo iliyopigwa Morogoro ilizikutanisha timu za Mwamnyeto Foundation na Morogoro Combine, gemu hiyo ilitamatika kwa sale ya bao 2-2.

Timu zote mbili zilisheheni Mastaa kibao lakini kivutio kikubwa kwa timu hizo ni Winga wa Moro Combine Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe Aziz Abood anayetajwa kuwa tajiri namba moja mkoani Morogoro aliyeichachafya vilivyo ngome ya Mwamnyeto Foundation.

Kwa Upande wa  Mwamnyeto Foundation kivutio kikubwa alikuwa mchezaji kipenzi cha wana Simba Clatous Chota Chama’Mwamba wa Lusaka’ Raia wa Zambia.

Licha ya upinzani wa Jadi wa Simba na Yanga lakini wachezaji wawili wa Simba, Chama na Mzamiru  Yassin ‘Selemba’walikubali ombi la wachezaji hao wa Yanga kushiriki kwenye mchezo huo kwa lengo kuwasapoti.

Mgeni rasm kwenye mchezo huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Adam Kigoma Malima ambaye baada ya kukagua timu zote mbili alipiga Picha ya pamoja na wamiliki wa taasisi hiyo, Zawadi Mauya Maarufu ‘Gift Mauya’kushoto na Mwamnyeto[kulia].

Mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo Mtandao huu uliahadi kurusha hewani picha za matukio ya Mh Abood ambaye ni mchezaji wa kutumainiwa na timu ya Morogoro Veterani.

Kwa bahati mbaya kabla ya kufanya hivyo tajiri huyo anayemiliki Viwanja, Mabasi, Malori na Vyombo vya habari alipata msiba wa kufiwa na Mpendwa Mama yake Mzazi.

 Hivyo busara zilimuongoza Mwandishi wa Mtandao huu kusitisha kwa muda habari hiyo akiungana na familia ya Mh Abood kuomboleza kifo hicho.


No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...