Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, August 9, 2023

M.C MAARUFU DAR AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI.

Mwili wa Marehemu ukitolewa ndani naq kuweka eneo la lbada.

                  Kiongozi wa Jumuiya akisoma eneo la Pili
                         Mc Herman akifungua Jeneza

               Siasa 'Mama Jamillah' akimuaga jirani yake
Kiongozi wa Madereva wa Treni Mkoa wa Morogoro naye akitoa heshima zake za mwisho
Afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania 'JWTZ; Kanali Deo akumuaga mpendwa bibi yake
Makamo Mwenyekiti wa Tawi kuu la Simba Mkoa wa Morogoro Samora Frank akitoa heshima za mwisho
              Marehemu Samole enzi za Uhai wake
Mc Herman[kushoto] na Mdogo wake Richard wakimuaga mpendwa mama yao huku wakiwa wamekumbatiana ikiwa ni ishara ya Upendo.

Padre akitoa Mahubiri hayo yaliyowagusa waislamu na wakristo.


Adella Mdede akimuaga Mpendwa Mama yake kwa kilio kizito,huku akisaidiwa na Katibu Mkuu wa CCM Kata ya Mji Mpta Mary Kunambi[kushoto]

Msiba huu ulikuwa nyumbani kwa Marehemu Mji Mpya Jirani na tawi la Simba la Shujaa

 


         Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 Mshehereshaji’M.C Maarufu Mkoa wa Dar es salaam  Mc.Herman Mdede ambaye pia ni Askari Polisi amepata pigo kubwa la kufiwa na Mama yake Mzazi Marehemu Salome Mdede[87].

Marehemu Salome aliyezaliwa June 7-1936 na kufariki  Julai 6-2023 amezikwa Jana Julay 8  Makaburi ya Kolla Mkoani Morogoro.

 Umati mkubwa wa watu wenye Imani tofauti za dini walishiriki imada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Mji Mpya.

 Kufuatia wingi wawatu hao wa dini za kikristo na Kiislam kwenye Mahubiri yake Padre aliyeongoza Misa hiyo alitoa mahubiri yaliyogusa waumini wa dini hizo, akisema.

“Licha ya tofauti zetu za kidini lakini  sote tunaamini Mungu ni Mmoja, sisi wa Kristo tukifuatia mafundisho ya Yesu Kristo na wenzetu Waisalam wakifuata mafundisho ya Mtume Muhammad.

Mitume hiyo inatufundisha kutenda mambo mema ikiwemo ya kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa waislama na Kwarezima kwa wakristo.

Lakini utashangaa baadhi ya waislam wachache Mwenzi Mtukufu hawafungi na hana tatizo lolote kiafya unajiuliza huyu mtu kajiumba mwenyewe?.

Au utashangaa kwa mujibu wa lmani ya dini ya Kiislamu huruhusiwi kula Kiti Moto lakini kwenye mabanda ya kiti Moto tunashangaa kuwaona waislamu wakila Kiti Moto”alisema Padre huyo na kupokea zawadi ya Makofi kutoka kwa waumini wa dini hizo.

Baadhi ya watu mashuhuri walishuhudiwa na Mwandishi wa Mtandao huu Msibani hapo ni pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Morogoro Doroth Mtenga, aliyekuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Mkoa wa Morogoro Mh Mama Saduka, ambaye kwa sasa ni kigogo wa CCM Kata ya Kilakala.

Diwani wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM Sabra ‘Mwarabu’.

Wengine ni Afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania’JWTZ’ Kambi ya Nyumbu Kibaha Kanali Deo,na kundi la Madereva wa Treni Mkoa wa Morogoro.

Marehemu Salome ameacha watoto watano, wa kwanza Adella Mdede’Mrs Mlowa ambaye ni Mwalimu Mstaafu.

Wapili Blandina Mdede, Mjasiliama.

Wa tatu Herman Mdede’Askari Polisi Dar es salaam.

Richard Mdede, dreva wa Treni Mkoa wa Morogoro. na Juliana Mdede. Mjasiliama.

 lfahamike Mwandishi wa Mtandao huu amesoma shule ya Msingi na Mc Herman pamoja na Kanali Deo, ambaye Marehemu Salome ni bibi yake.

Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kadhaa kwenye msiba huo ikiwemo tukio la babu wa Shiza Kichuya kutinga msibani na jezi ya Namungo.

Endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

                       

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...