Hayati Mumba enzi za Uhai wake
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
TIMU ya Mtibwa Sugar yenye Mskani yake katikati ya Mashamba ya Miwa eneo la Manungu Kata ya Mtibwa Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, wamefunguka mazito kifo cha Mwalimu Maarufu wa Mpira wa Miguu Tanzania Kocha Ahmedi Mwarabu Mumba.
Baada ya kutokea kwa Msiba huo mzito,Uongozi wa Mtibwa uliotuma wawakilishi wawili kuja Morogoro Mjini kushiriki mazishi hayo.
Akizungumza na Mtandao huu juzi nyumbani kwa marehemu Kihonda Mbuyuni Kata ya Mafisa, Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano cha Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligarambwike amesema.
” Shekidele Uongonzi wa Juu wa timu yetu umenituma mimi na mwenzangu kuja kushiriki msiba huu mzito wa Kocha Mumba.
Ifahamike Kocha Mumba ndiye kocha aliyeipandisha daraja timu yetu mwaka 1995 tukitokea ligi daraja la kwanza kuingia ligi kuu, miaka 4 mbele kwa maana ya 1999 na 2000 tulifanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania bara mara mbili mfurulizo kocha Mumba akiwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio hayo.
Kama hiyo haitoshi toka tupande daraja 1995 hatujashuka daraja mpaka sasa tunaendelea kukipiga Ligi kuu miaka 28 mfurulizo kwa Mantiki hiyo ukitoa Simba na Yanga sisi mtibwa ndio timu kubwa ”alisema Afisa habari huyo mwenye maneno mengi.
Mbali na Mtibwa Sugar Mwandishi wa Mtandao huu anazikumbuka timu nyingine alizozipandisha daraja Kocha Mumba ni Mirambo ya Tabora, Nazareti ya Njombe, na Polisi Morogoro.
No comments:
Post a Comment