Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, August 29, 2023

MAMIA YA WANANCHI WAMEJITOKEZA KWA WINGI KUMZIKA MKUFUNZI WA MAKOCHA TANZANIA.



 Mh Fikiri akitabasamu baada ya kukumbushwa jambo na Mwandishi wa Mtandao huu ambapo kuna kijiweo chetu cha kunywa chai Pricens hotel imekufa kwa sasa tunakutana Bums nyakati za jioni.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe Fikiri Juma ambaye pia ni mdau mkubwa wa Soka akitoa salamu zake za rambi rambi.

Kiongozi wa chama cha wachezaji wa zamani [UMSOTA Tanzania] Hamisi Malivedha kulia akimkabidhi rambi rambi Mwarabu Mumba ambaye ni mtoto wa marehemu Ahmed Mumba.[11] Mratibu wa Moro Kids Rajab Kindagule[kulia akikabidhi rambi rambi kwa niaba ya kituo hicho cha Moro Kids kinachoongoza kutoa wachezaji nyota wanaota,mba kwa sasa ligi kuu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro'MRFA' Emmanuel Kimbawara akitoa saramu za rambi rambi." Kama mnavyojua Marehemu Mumba alikuw amkufunzi wa makocha hata Tanzania,hivyo Rais wa TFF Wales Karia amenituma kutoa saramu hizi za rambirambi kwa msiba huu mzito kwa familia ya wanasoka,"alisema Katibu huyo ambaye Mchungaji Mstaafu wa makanisani ya Sabato


Mwarabu Mumba mtoto wa kiume wa marehemu Ahmed Mumba akitoa neno la shukrani.

" Nawashukuru wote waliotukimbilia kwenye msiba huu mzito wa Mpendwa baba yetu, kipekee nimshukuru Mhe Abood Mbunge wetu wa jimbo la Morogoro ambaye ndiye aliyetoa gari lililobeba mwili wa baba kutoka Dar Mpaka hapa nyumbani,

 kama hiyo haitoshi kato sanduku lililobeba mwili pamoja na kilo 50 za mchele"alisema Mwarabu Mumba ambaye ni Mwamuzi Mwandamizi wa ligi daraja la kwanza taifa aliwahi pia kucheza ligi kuu


Afisa habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligarambwike kitabasamu baada ya kumuona Mwandishi wa Mtandao huu, Picha no 2 Kifaru akiteta jambo na Mwamuzi Mstaafu

. Akizungumza na Mtandao huu Kifaru amedai ametumwa na Uongozi wa Mtibwa Sugar kuhudhuria msiba huo akidai marehemu Mumba anahistoria kubwa na timu hiyo

Historia hiyoitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote

Kutoka kulia.

Hamis Kambi, Mwamuzi Mstaafu ambaye ni Askari Magereza wa gereza kuu la Manispaa ya Morogoro.Ally Jangalu. Kocha wa zamani wa Kagera Sugar. Mwalimu Mzigira kocha wa zamani wa Reli Morogooro.Thobias Kifaru Ligarambwike, Afisa habari wa Mtibwa Sugar. Hasani Gobosi’Gadagada’ Kocha wa zamani wa Reli ya Morogoro.Mwisho aliyesimama ni Athuman Matenga Katibu Msaizidi  Reli ya Morogoro ‘Kiboko cha Vigogo’.

 

Wadau wa soka kutoka Kushorto ni Afande Hamis Kambi, Afande Salum Mbaruku ambaye ni mchezaji wa zamani wa Mirambo ya Tabora na Polisi ya Morogoro. Thibias Kifaru Afisa habari Mtibwa Sugar, mwenye kofia nyeusi ni Mgosi mwalimu mwaafudu wa madereva akipiga kazi Morogoro Dreving School 

pembeni yake ni Afande Daud Salum huyu ananyazifa kibao. ni mwenyekiti Msaafu wa timu ya Polisi Mara, Katibu Mstaafu wa chama cha Soka Mkoa wa Mara, Mjumbe wa timu ya Polisi Morogoro,

Baada ya kustaafu Upolisi katimkia kwenye siasa na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata ya Mafisa labla ya kuangukia pua kwenye uchaguzi mkuu uliopita akishindwa na Mh Kizomi Maarufu Dr wa Mifupa anayemiliki hospital ya Mifupa eneo hilo la Mbuyuni kata ya Mafisa.

Wa mwisho mwenye kofia nyeupe Mwandishi wa Mtandao huu hakuweza kumfahamu fasta.

 


Athuman Kairo kocha wa zamani ya Pamba ya Mwanza kwenye msiba huo alikuwa mratibu wa mambo yote loicha ya marehemu kuwa mwalimu wake wa Ukocha lakini pia wanatoka Mkoa mmoja wa Kigoma

Mmiliki wa shule za Mteule Open School zilizopo Uwanja wa Jamhuri Morogoro na Sanga sanga njia panda ya Mzumbe. Mteuke ni mdau mkubwa wa soka akiishabikia timu ya Simba










         Marehemu Mumba enzi za Uhai wake

                Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MAMIA ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali nchini wakiongozwa na msemaji mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligarambwike, jana wamejitokeza kwa wingi kumzika Mkufunzi  wa Makocha Tanzania Marehemu Ahmed Mumba.

Marehemu Mumba ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Makocha Mkoa wa Morogoro’TAFCA’  amefariki dunia Jumamosi iliyopita hospital ya Mloganzira Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa jana Makaburi ya Kolla Mkoani Morogoro.  

Mara baada ya Kocha Mumba kufariki  Mwili wake ulirejea nyumbani kwake Kihonda Mbuyuni Kata ya Mafisa ambapo wadau mbali mbali wa soka wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma wamefulika nyumbani kwa marehemu kushiriki lbada ya kumuombea  iliyoongozwa na Mashehe zaidi ya 7.

Wingi wa Mashehe hao unatokana na Marehemu Mumba enzi za uhai wake kuwa jirani na Mwenyezi Mungu kwa kushiriki  swala 5 kwenye misikiti mbali mbali ya Mkoa wa Morogoro.

Baadhi ya Mashehe hao ni pamoja na Shehe Koba wa Msikiti wa I.G.P Mstaafu Alhaj Omar ldd Mahita ulipo Mafiga, Shehe Ally Omar wa Msikiti Mkuu wa Morogoro ulipo Boma Road.

Wengine ni Shehe Shaban Juma wa Msikiti wa Awayya Uliopo Mawenzi ambaye ndiye aliyepiga Adhana swala ya saa 10 iliyofanyika nyumbani kwa  marehemu akitanguliwa na swala ya kumuombea Marehemu yenye lakaa 4.

Enzi za uhai wake Marehemu Mumba akiwa katibu wa TAFCA huku mwenyekiti wake akiwa John Simkoko chama hicho kinatambuliwa na shirikisho cha Mpira wa Miguu Afrika’CA F’.

Hivyo Hayati Mumba na Simkoko mara kwa mara kupitia chama  hicho walitoa mafunzo ya ukocha yanayotambuliwa na CA F,makocha kibao wakiwemo wa Simba,Yanga Azam wameshiriki mafunzo hayo na kukabidhiwa leseni zinazotambuliwa na CA F na Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.

 Baadhi ya makocha hao ni Pamoja na Seleman Matola, Simba Abibu Kondo Mtibwa Sugar Mecky Mexime Kagera Sugar, John Tamba, Polisi Tanzania,Zuberi Katwira Ihefu.

Wengine ni Juma Kaseja, Ulimboka Mwakingwe, Athuman Kairo Ally Jangalu.na  Bi.Edina Lemma aliyekuwa kocha wa Yanga Princess

Kama kawaida Mwandishi wa Mtandao huu alizunguka kona zote kwenye msiba huo akisaka picha za watu maarufu alizosiona hapo juu


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...