Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, August 10, 2023

MC MDEDE ALIZA WATU MSIBANI AKIMSIHI MDOGO WAKE KUMUGA MPENDWA MAMA YAO.




lnauma sana Herman[kulia] akimsihi mdogo wake Richard kutazama kwa mara ya mwisho sura ya Mpendwa mama yao aliyelala ndani ya jeneza hata hivyo Rich aligoma kabisa kumtzama mama yake


Afande Mdede akifuta machozi baada ya kumuaga mpendwa Mama yake
Richard akinyoosha kidole juu kuashiria kushiri sakrameti takatifu
Afande Herman Mdedekushoto] akiwa sambamba na mdogo wake Richard Mdede kabla ya zoezi la kuaga mwili kuanza
Mc Mdede akiweka shada la Mau kwenye kaburi la Mpendwa Mama yake

Baadhi ya waombolezaji wakiwa ndani ya tawi kuu la Simba ,ambalo liko jirani kabisa na nyumba ya marehemu Salome


                         Muonekano wa Juu eneo hilo la Msiba

 

            Na Dustan Shekidele,Morogoro.

INAUMA SANA. Mc Maarufu Mkoani Dar es salaam Afande Herman Mdede juzi aliliza baadhi ya waombolezaji pale alipobeba jukumu la Kumbembeleza Mdogo wake Richard Mdede  ajikaze na kumuaga Mpendwa Mama yao Marehemu Salome Mdede.

 Richard Maarurfu ‘Make’[Pichani kulia mwenye shati jeupe]ambaye ni dreva wa Treni Shirika la Reli Mkoa wa Morogoro alikubari ombi la Kaka yake huyo ambaye ni Askari Polisi Mkoa wa Dar es salaam.

Wakati wakielekea kwenye jeneza  huku wakikumbatiana kwa upendo wakiimba wimbo wa dini,Richard alipokaribia aligoma kumuangalia Mpendwa mama yake na kugeuza kichwa chake pembeni. 

Afande Herman alimsihi sana mdogo wake  kama anavyoonekana Pichani, lakini Richi  alishikiria Msimamo wake wa kugoma kumtazama Mama yake akiwa amelala ndani ya Sanduku.

Safari ya kuelekea Makaburi ya Kolla kumpunzisha Mpendwa mama yetu kwenye nyumba yake ya milele ilianza, tulipofika Padre aliongoza Misa ya Mazishi ambapo Richard alishiriki kikamilifu Misa hiyo, ilipofika tamati mwili iliingizwa kaburini na kuanza kufukiwa.

 Zoezi hilo lilipoanza Richard alimfuata Mwandishi wa Mtandao huu na kumueleza kwamba hawezi kutazama Mama yake akifukiwa na Mchanga.

”Shekidele siwezi kuangalia Mama yangu niliyempenda akifukiwa na kufusi cha Mchanga Presha inapanda naweza na mimi nikaanguka hapa Makaburni naomba nisindikize barabarani nichukue boda boda nirudi nyumbani”alisema  huku akihema kwa shinda kufutia mapigo yake ya moyo yakienda kasi.

Wakati wa kuweka mashada ya Mau Afande Mdede aliyekuwa Mc kwenye zoezi hilo alianza kwa kuwaalika watoto wa kike ya Marehemu ambao ni Adella, Blandina na Juliana.

Ratiba ilionyesha wanaofuta kuweka shada la Maua ni watoto wawili wa marehemu ambao ni Herman na Richard hivyo Mc Mdede aliweka Mic Pembeni akashika Ua na kumwalika Mdogo wake ambaye awari amimshuhudia eneo hilo la Makaburi.

Mwandishi wa habari hizi alitumia busara ya kueleza waombolezaji kwamba Richard amepata dharura ametoka kidogo, baada ya taarifa hiyo Herman aliweka shada hilo kama anavyoonekana Pichani.

Baada ya taarifa hiyo baadhi ya  watu  wakiona ni jambo la tofauti lakini kwa  sisi tunayefahamu afya ya Richard hatukushangaa.

Wasomaji wa Mtandao huu watakumbuka siku za nyuma  niririrpoti hatari ya Richard Mdede kuanguka na kupoteza fahamu kwenye tawi kuu la Yanga wakati akiangalia mpira wa Simba na Yanga.

Dreva huyo wa Treni ni shabiki lia lia wa Simba huku marafiki zake wengi waki shabikia Yanga, hivyo kwenye gemu hiyo  licha ya tawi kuu la Simba kuwa jirani na nyumbani kwake aliamua kwenda kuangalia Daby hiyo kwenye  la Yanga lililpo Mtaa wa tatu kutoka nyumbani kwake lilipo tawi la Simba.

Baada ya shuti kali la Aziz K kutinga wavuni na kumuacha Kipa wa Simba Aishi Manura akidaka hewa, Richard Pesha ilipanda akanguka chini na kupoteza fahamu.

Mashabiki hao wa Yanga walikimbilia kumvua Viatu huku wakimpepea kisha kumkimbiza  Zahanati ya Kata ya Mji Mpya iliyopo hatua 5 kutoka tawi hilo la Yanga.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga walimpigia simu Mwandishi wa habari hizi ambaye fasta alitinga kwenye Zahanati hiyo na kumshuhudia dreva huyo wa Tren akiwa hoi bintaabani Presha ikiwa juu zaidi.

Alipatiwa huduma ya kwanza kisha akapewa Rufaa ya kwenda hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro alikopatiwa matibabu na kurejea katika hali yake ya kawaida huku akishauri na Madaktari  asiangalia  Mpira ‘Live’kwenye Tv.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...