Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, August 11, 2023

BABU KICHUYA ATINGA MSIBANI NA JEZI YA NAMUNGO.

Mzee lbrahimu Mangwende'Babu Kichuya' akiwa na uzi wa Namungo Fc
Mc Herman Mdede[kulia] akiongoza ndugu na Jamaa kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Mpendwa Mama yake, kushoto Babu kichuya akifutilia kwa umakini mkubwa tukio hilo
 


             Na Dustan Shekidele,Morogoro.

lbrahim Mangwende ‘Maarufu babu Kichuya’Juzi ametinga Msibani akiwa na jezi ya timu ya Ligi Kuu ya Namungo yenye Maskani yake Luangwa Mkoani Lindi.

Mzee huyo ambaye ni babu Mzaa Mama wa Mchezaji nyota nchini Shiza Ramadhan Kichuya anayekipiga Namungo Fc, alivaa Uzi huo ulioandikwa nyuma’Kichuya’ kwenye Msiba wa Marehemu Salome ambaye ni Mama mzazi wa Mc Maarufu Mkoani Dar es salaam Afande Herman Mdede.

lfahamike binti wa Mzee huyo,ambaye ametangulia mbele za haki, tukizidikumuombea kwa Mwenyezi Mungu amrehemu, kwenye uzao wake alijifungua watoto  watatu kwa Mpigo, Kulwa, Dotto na Shiza, Kulwa na Dotto walifariki dunia wakimfuata Mpendwa Mama yao, huku Mwenyezi Mungu akimbakiza Shiza anayeendelea kuifariji familia hiyo.

Kulwa na Mama yake tuliwazika Makaburi ya Kolla huku Dotto tukimzika Makaburi ya Mafisa kwa Mambi.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...