Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, August 14, 2023

MAMIA YA WATU WAMZIKA SEKRETARY KIONGOZI WA KIWANDA CHA TUMBAKU

                           Catherine Mapunda enzi za Uhai wake



Mc Maarufu Mkoani Morogoro ambaye ni Askari Polisi mwenye nyota kadhaa begani akimuamuru Mtaalamu kuingiza jeneza lililobeba mwili wa Mpendwa wetu kaburini kwa kutumia mashine Maalumu.


....Mtaalamu akiingia jeneza hilo kaburi kwa mashine maalumu



Mume wa Marehemu Dkt Mosi akiweka shada la Maua kwenye kaburi la Mpendwa Mke wake
Mkurugezi wa Kiwanda cha Mkwawa Mzungu akiweka shada la Maua kwenye kaburi la mfanyakazi wake.

 

 

           Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Wiki iliyopita Mji wa Morogoro uligubikwa na Simanzi kufuatia kifo cha ghafra cha Kigogo wa Kiwanda cha Tumbaku kilichopo Morogoro Mjini eneo la lringa Road Marehemu Catherine Mapunda.

 Marehemu Catherine [Maarufu Dada Ketty]aliyekuwa Katibu Muhtasi[Sekretary] wa Mkurugenzi wa Kiwanda hicho ambacho kwa sasa kinajulikana kwa jina la Mkwawa Tobacco alifariki Agosti 6 na kuzikwa Agost 9 Makaburi ya Kolla.

Umati mkubwa wawatu ulifurika Msibani nyumbani kwa Marehemu Bigwa barabara ya zamani ya Dar es salaam, baadae umati huo ulishiriki lbada Maalumu ya kumuombea iliyofanyika kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Parokia ya Mwili na Damu Bigwa.

Baada ya lbada hiyo kukamilika Msafara wa kuelekea Makaribu ya Kolla kumpunzisha Mpendwa wetu ilianza kwa msafara wa magari na Pikipiki zikiongozwa na Pikipiki ya Mwandishi wa Mtandao huu.

UHUSIANO WA MAREHEMU NA MWANDISHI WA MTANDAO HUU.

Takribani miaka 6 sasa Mpiga Picha mashuhuri wa Mtandao huu anayemiliki kamera za kisasa ndiye anayewapiga Picha za Passpoti Size Mabosi wote wa Kiwanda hicho wakiwemo Wazungu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kiwanda.

Ilipohitajika Mzungu kupiga Picha Dada Ketty alinipigia simu, kufuatia hali hiyo ya kwenda mara kwa mara kiwandani hapo kwa Mwaliko wa Catherine walinzi wote wa kiwanda hicho walinifahamu hivyo nilipita kwenye mageti yote mawili lile la kiwandani na kile la Ofisini kama Staff wa Kiwanda.

Licha ya Catherine kuwa Boss Lady wangu pia tulikuwa tukiitana Kaka na Dada kwani sote tunatokea mkoa mmoja wa Tanga.

lfahamike baba mzazi wa Marehemu Catherine Mzee Mapunda alikuwa Mngoni wa’Kunyumba’ kutoka Mkoa wa Ruvuma huku Mama yake mzazi  Msambaa wa Korogwe Mkoa wa Tanga na Marehemu alizungumza vizuri Lugha ya Kisambaa.

Mara ya mwishoni kuwasiliana na Mpendwa wangu Dada Catherine ni mwishoni mwa mwezi wa 7 kama kawaida alinipigia simu akinieleza  kuna Mzungu anahitajika kupiga Picha  fasta nilikwenda kiwandani kufanya kazi hiyo. 

Agost 4 nilimpigia simu nikiwa na shida naye binafsi simu yake iliita bila kupokewa  nikahisi yuko kwenye kikao, mara nyingi akiona Mic Call yangu lazima apige.

Safari hii nimeshangaa hakupiga siku 3 mbele simu yangu ikaita nilipoangalia nikaona jina la dada Cathe nilipoipokea kikashangaa kusikia sauti ya mtu mwingine ikisema,

”Mimi ni dada yake Catherine na simu yake ninayo mimi  Catherine hatunaye tena amefariki dunia”

Baada ya kusikia taarifa hizo zilizorarua Moyo wangu nilisikia maumivu Makali yatiyoanzia kwenye nyayo za Miguu mpaka kwenye utumbo, usmati nikauweka kando nikaketi kwenye vumbi na kujiuliza maswali kama kweli taarifa hizo ni za kweli au naota ndoto ya mchana.

 Nikapata majibu kwamba kuthibitdhs taarifa hizo nifike nyumbani kwa dada Catherine, hivyo niliitia sauti hiyo nikapiga gia Pikipiki yangu hadi nyumbani kwa  mpendwa dada yangu. Nilipokaribia niliona magari mengi nje ya nyumba yake nikaanza kuamini nilipovuka geti na kuingia ndani nimeshuhudia watu wameketi chini ya maturubai huku nyimbo za maombelezo sauti ya chini zikitawara eneo hilo.

Nikaangalia kuliana na kushoto nikawaomba wazungu wengi wa kiwanda hicho na wafanyazi wengine nilipotupa jicho kushoto nikamuona Mume wa Marehemu Dkt Mosi  akiwa na nguo nyeusi nilisoge na kumpa mkono wa pole.

Mbele yangu Nikaona Picha kubwa ya Mpendwa dada yangu, nikashindwa kujizuia na kujikuta natokwa na machozi  ya uchungu

“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe”

               


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...