Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, August 3, 2023

FAMILIA YASIMULIA KIFO CHA MKURUGENZI WA KATIBA.

Msemaji wa familia  Bw Mzeru akihojiwa na Mwandishi wa Mtandao huu


               Nyumbani kwa Marehemu Kijiji cha Lukenge
                             Mwili ikiwasiri kwenye kaburi

Mzeru na familia yake wakiweke shada la Mau kwenye kaburi la Mpendwa mdogo wake.

            Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Msemaji wa Familia aeleza A-Z kifo cha Mpendwa wao Marehemu Khalist Michael Luanda[57] Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria.

Baada ya kutokea kwa kifo hicho Julai 27 jijini Dar es salaam na Marehemu kuzikwa Julai 31  nje ya nyumba yake iliyopo Kijijini kwake Lukenge eneo la Dabwala Kata ya Kibungo Juu  Tarafa ya Matombo Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoani hapa.

 Mwandishi wa Mtandao huu alifunga safari hadi kijijini hapo na kushiriki Mazishi ya Mpendwa wetu huyo aliyejaliwa kuishi vizuri na watu licha ya  Cheo chake na usomi wake.

Hali hiyo ilidhibitishwa kwenye Mazishi yake ambapo umati mkubwa wawatu ulifulika huku wengi wakitokea Mikoa ya Dodoma,Dar es Salaam, Morogoro Mjini na kijijini hapo.

Akizungumza kwenye Mahojiano Maalumu na Mwandishi wa habari hizi Msemaji wa familia Bw Lungine Mzeru[Pichani] ambaye ni Kaka wa Marehemu alipotakiwa kueleze kifo hicho cha Mdogo wake alisema.

” Julai 20 Mdogo wake alitoka nyumbani kwake Dodoma akaaga familia yake kwamba anakwenda  Muhimbili kwenye matibabu ya Jicho akadai atalala Morogoro julai 21 atanza safari ya kwenda Dar.

Asubuhi ya Julai 21 wakati akijiandaa  kwenda Dar Presha ilipanda akaanguka chumbani Majirani wakamkimbiza hospital ya Mkoa wa Morogoro, familia tulijurishwa mkewe alifunga safari kutoka Dodoma  na Mimi ninayeishi Gongola Mboto Dar nilifunga safari ya kuja hapa Moro,”alisema Msemaji huyo na kuendelea kusimulia.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya Julai 23 tulipewa rufaa ya kwenda Dar Mlonganzira akaendelea na matibabu  Julai 27 Mdogo wangu alifariki dunia, Msiba ulikuwa kwangu Gongola Mboto, baadae tukausafiri mwili hadi nyumbani kwake Dodoma ambapo watu mbali mbali wakiwemo wafanyakazi wenzake walipata nafasi ya kumuaga.

Baada ya zoezi hilo kukamilika tulianza safari ya kuja hapa nyumbani Morogoro Kijijini kwetu Lukenge kumpunzisha mpendwa wetu kwenye nyumba yake ya Milele”alisema Bw Mzeru.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.

“Mwendo umeumaliza Mpendwa wetu nenda salama Kamanda tutaonana baadae”.

Baadhi ya matukio ya msiba huo Mwandishi wa habari hizi pia ameyarusha  gazeti la Raia Mwema la jana ambalo mpaka sasa bado liko Mtaani unaweza kulipitia.

 Kwenye salamu zake za Rambi rambi Naibu Waziri wa Katiba na Sheri kumtaja Marehemu Luanda  kuelekea Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya unaotarajiwa kuanza hivi karibuni,endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.


 

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...