Mh
Fikiri akitabasamu baada ya kukumbushwa jambo na Mwandishi wa Mtandao huu
ambapo kuna kijiweo chetu cha kunywa chai Pricens hotel imekufa kwa sasa
tunakutana Bums nyakati za jioni.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe Fikiri Juma ambaye pia ni mdau mkubwa wa
Soka akitoa salamu zake za rambi rambi.
Kiongozi wa
chama cha wachezaji wa zamani [UMSOTA Tanzania] Hamisi Malivedha kulia
akimkabidhi rambi rambi Mwarabu Mumba ambaye ni mtoto wa marehemu Ahmed Mumba.[11]
Mratibu wa Moro Kids Rajab
Kindagule[kulia akikabidhi rambi rambi kwa niaba ya kituo hicho cha Moro Kids
kinachoongoza kutoa wachezaji nyota wanaota,mba kwa sasa ligi kuu
Katibu Mkuu
wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro'MRFA' Emmanuel Kimbawara akitoa saramu za
rambi rambi." Kama mnavyojua Marehemu Mumba alikuw amkufunzi wa makocha
hata Tanzania,hivyo Rais wa TFF Wales Karia amenituma kutoa saramu hizi za
rambirambi kwa msiba huu mzito kwa familia ya wanasoka,"alisema Katibu
huyo ambaye Mchungaji Mstaafu wa makanisani ya Sabato
Mwarabu
Mumba mtoto wa kiume wa marehemu Ahmed Mumba akitoa neno la shukrani.
"
Nawashukuru wote waliotukimbilia kwenye msiba huu mzito wa Mpendwa baba yetu,
kipekee nimshukuru Mhe Abood Mbunge wetu wa jimbo la Morogoro ambaye ndiye
aliyetoa gari lililobeba mwili wa baba kutoka Dar Mpaka hapa nyumbani,
kama hiyo
haitoshi kato sanduku lililobeba mwili pamoja na kilo 50 za
mchele"alisema Mwarabu Mumba ambaye ni Mwamuzi Mwandamizi wa ligi daraja
la kwanza taifa aliwahi pia kucheza ligi kuu
Afisa habari
wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligarambwike kitabasamu baada ya kumuona
Mwandishi wa Mtandao huu, Picha no 2 Kifaru akiteta jambo na Mwamuzi Mstaafu
.
Akizungumza na Mtandao huu Kifaru amedai ametumwa na Uongozi wa Mtibwa Sugar
kuhudhuria msiba huo akidai marehemu Mumba anahistoria kubwa na timu hiyo
Historia
hiyoitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda
wote
Kutoka
kulia.
Hamis Kambi,
Mwamuzi Mstaafu ambaye ni Askari Magereza wa gereza kuu la Manispaa ya
Morogoro.Ally Jangalu. Kocha wa zamani wa Kagera Sugar. Mwalimu Mzigira kocha
wa zamani wa Reli Morogooro.Thobias Kifaru Ligarambwike, Afisa habari wa Mtibwa
Sugar. Hasani Gobosi’Gadagada’ Kocha wa zamani wa Reli ya Morogoro.Mwisho
aliyesimama ni Athuman Matenga Katibu Msaizidi Reli ya Morogoro ‘Kiboko cha Vigogo’.
Wadau wa
soka kutoka Kushorto ni Afande Hamis Kambi, Afande Salum Mbaruku ambaye ni
mchezaji wa zamani wa Mirambo ya Tabora na Polisi ya Morogoro. Thibias Kifaru
Afisa habari Mtibwa Sugar, mwenye kofia nyeusi ni Mgosi mwalimu mwaafudu wa
madereva akipiga kazi Morogoro Dreving School
pembeni yake
ni Afande Daud Salum huyu ananyazifa kibao. ni mwenyekiti Msaafu wa timu ya
Polisi Mara, Katibu Mstaafu wa chama cha Soka Mkoa wa Mara, Mjumbe wa timu ya
Polisi Morogoro,
Baada ya
kustaafu Upolisi katimkia kwenye siasa na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata ya
Mafisa labla ya kuangukia pua kwenye uchaguzi mkuu uliopita akishindwa na Mh
Kizomi Maarufu Dr wa Mifupa anayemiliki hospital ya Mifupa eneo hilo la Mbuyuni
kata ya Mafisa.
Wa mwisho
mwenye kofia nyeupe Mwandishi wa Mtandao huu hakuweza kumfahamu fasta.
Athuman
Kairo kocha wa zamani ya Pamba ya Mwanza kwenye msiba huo alikuwa mratibu wa
mambo yote loicha ya marehemu kuwa mwalimu wake wa Ukocha lakini pia wanatoka
Mkoa mmoja wa Kigoma
Mmiliki
wa shule za Mteule Open School zilizopo Uwanja wa Jamhuri Morogoro na Sanga
sanga njia panda ya Mzumbe. Mteuke ni mdau mkubwa wa soka akiishabikia timu ya
Simba
Marehemu Mumba enzi za Uhai wake
Na Dustan
Shekidele,Morogoro.
MAMIA ya
wananchi kutoka maeneo mbali mbali nchini wakiongozwa na msemaji mkuu wa timu
ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligarambwike, jana wamejitokeza kwa wingi
kumzika Mkufunzi wa Makocha Tanzania
Marehemu Ahmed Mumba.
Marehemu
Mumba ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Makocha Mkoa wa Morogoro’TAFCA’ amefariki dunia Jumamosi iliyopita hospital ya
Mloganzira Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa jana
Makaburi ya Kolla Mkoani Morogoro.
Mara baada
ya Kocha Mumba kufariki Mwili wake ulirejea
nyumbani kwake Kihonda Mbuyuni Kata ya Mafisa ambapo wadau mbali mbali wa soka
wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma
wamefulika nyumbani kwa marehemu kushiriki lbada ya kumuombea iliyoongozwa na Mashehe zaidi ya 7.
Wingi wa
Mashehe hao unatokana na Marehemu Mumba enzi za uhai wake kuwa jirani na Mwenyezi
Mungu kwa kushiriki swala 5 kwenye
misikiti mbali mbali ya Mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya
Mashehe hao ni pamoja na Shehe Koba wa Msikiti wa I.G.P Mstaafu Alhaj Omar ldd Mahita
ulipo Mafiga, Shehe Ally Omar wa Msikiti Mkuu wa Morogoro ulipo Boma Road.
Wengine ni Shehe
Shaban Juma wa Msikiti wa Awayya Uliopo Mawenzi ambaye ndiye aliyepiga Adhana
swala ya saa 10 iliyofanyika nyumbani kwa
marehemu akitanguliwa na swala ya kumuombea Marehemu yenye lakaa 4.
Enzi za uhai
wake Marehemu Mumba akiwa katibu wa TAFCA huku mwenyekiti wake akiwa John
Simkoko chama hicho kinatambuliwa na shirikisho cha Mpira wa Miguu Afrika’CA F’.
Hivyo Hayati
Mumba na Simkoko mara kwa mara kupitia chama
hicho walitoa mafunzo ya ukocha yanayotambuliwa na CA F,makocha kibao
wakiwemo wa Simba,Yanga Azam wameshiriki mafunzo hayo na kukabidhiwa leseni
zinazotambuliwa na CA F na Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.
Baadhi ya makocha hao ni Pamoja na Seleman
Matola, Simba Abibu Kondo Mtibwa Sugar Mecky Mexime Kagera Sugar, John Tamba,
Polisi Tanzania,Zuberi Katwira Ihefu.
Wengine ni
Juma Kaseja, Ulimboka Mwakingwe, Athuman Kairo Ally Jangalu.na Bi.Edina Lemma aliyekuwa kocha wa Yanga
Princess
Kama kawaida Mwandishi wa Mtandao huu alizunguka
kona zote kwenye msiba huo akisaka picha za watu maarufu alizosiona hapo juu