Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, July 13, 2023

MKUU WA MKOA AFUNGUKA KUIMBA KWAYA HOTELINI

Mkuu wa Mkoa[kati] akishiriki kuimba na kwaya kurasni kwenye hoteli ya Glonency Morogoro 





                   ...Akipiga picha ta pamoja na wana kwaya hao
 


                                 Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MKUU wa Mkoa wa Njombe Mh Anthony Mtaka Wiki iliyopita ameshirki kuimba nyimbo za dini na Kwaya ya Kurasini Choir ndani ya hotel ya Glonency iliyopo Nane Nane Mkoani Morogoro.
 
Mkuu huyo wa Mkoa ambaye ni mlezi wa Kwaya hiyo Maarufu nchini inayotokea Kanisa la Wasabato Kurasini Jijini Dar es salaam ameonyesha kipaji cha hali ya juu cha uimbaji. 
 
Akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi mara baada ya kushiriki kuimba nyimbo zaidi ya 4 na Mkuu huyo wa Mkoa alisema.
“Shekidele kwanza ujue hii kwaya ni maarufu sana hapa nchini na nje ya nchini nyimbo zao nyingi zinatamba YouTube.
 
kwa miaka mingi mimi ni mlezi wa Kwaya hii”alisema Mkuu huyo wa Mkoa aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoa Morogoro kabla ya kupanda cheo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, baadae akahamishiwa jiji la Dodoma na hivi karibuni akahamishiwa Mkoa wa Njombe. 
 
Alipoulizwa kwamba ameonyesha kipaja cha hali ya juu cha kuimba nyimbo za kwaya hiyo bila kubabaika je nyimbo hizo amezijuaje ilihali yeye sio mwimbaji wa kwaya hiyo?.
 
”Kweli mimi sio Mwimbaji wa kwaya hii nazijui nyimbo zao kwa sababu kila albam mpya lazima nipate nakala moja na mara nyingi nikimaliza kazi zangu pale nyumbani au ofisini huwa nasikiliza nyimbo za kwaya hii ndio maana nyingi ziko kichwani”alisema Mtaka
 
Naye Katibu Mkuu wa Kwaya hiyo Jonhson Sebastian akihojiwa Mtandao huu alisema yamefika Mkoa Morogoro kwenye semina ya wiki Moja inayofanyika kwenye kanisa kuu la Wasabato Mkoa Morogoro.
 
”Baada ya kufika tukakutana na Mlezi wetu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Mtaka akatualika kuja hapa hotelini kula naye chakula cha jioni”alisema Katibu huyo. 
 
Hivi karibuni akishiriki kwenye mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya hayati Francis Leonard Mtenga aliyefariki dunia,Julai Mosi kwa ajari, baada ya kugongwa na Trekta[Power Tiller]Shambani kwake Mbarali na kuzikwa kijijini kwao Mkoani Njombe.
 
Mkuu wa Mkoa Mtaka alimmwagia sifa Hayati Mtenga kwamba enzi za uhai wake alijitoa kusaidia wanyonge sambamba na kujitoa kwenye shughuli za kanisa.
 
”Kuna baadhi ya watu wakifariki dunia Viongozi wa dini, wachungaji au Mashehe wanapata tabu kutafuta mema ya marehemu aliyoyafanya enzi za uhai wake baadhi ya viongozi hao wanalazimika kutunga Uongo kumpamba marehemu.
 
Lakini kwa Mh Mtenga hilo ni tofauti enzi za uhai wake sote ni mashuhuda alijitoa kusaidia ujezi wa nyumba za lbada hapa Njombe na kwenye jimbo lake”alisema Mkuu huyo wa mkoa kwenye lbada ya Mazishi ya Mbunge huyo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...