Mwandishi wa Mtandao huu licha ya kipato chake kidogo alipokea Neema ya Bwana ya Utoajia.
Pichani Mtumishi huyo wa Mungu akitoa Misaada kwa watu mbali mbali wenye uhitaji wakiwemo watoto yatima, akiamini kwamba hakuna Mtu aliyefirisika kwa kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Natumia maneno haya na Picha hizi kuwahamasisha na kuwakumbuha watu wengine kuwasaidia ndugu zetu wenye uhitaji na nisieleweke vinginevyo.
WAGALATIA 6.1-10.
“ Ndugu zangu mtu akighafilika katika kosa lolote,nyinyi mlio wa roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho upole,ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Mchukuliane Mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.
Maana mtu akijiona kuwa na kitu naye si kitu,ajidanganya nafsi yake.
Lakini kila mtu na ajipime kazi yake Mwenyewe ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu,wala si kwa Mwenzake.
Maana kila Mtu atalichukua furushi lake Mwenyewe.
Mwanafunzi na awashirikishe wakufunzi wake katika Mema yote.
Msidanganyike Mungu hadhihakiwi kwa kuwa chochote apandacho Mtu ndicho atakacho vuna.
Maana yeye apandaye kwa Mwili wake katika Mwili wake atavuna uharibifu,bali yeye apandaye kwa roho,katika roho atakuwa na Uzima wa Milele.
Tena tusichoke katika kutenda Mema,maana maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho.
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafsi na tuwatendee watu wote mema na hasa jamaa waaminio”.Hilo ndilo neno letu la Leo Jumapili ya Julai 16.
Leo sina cha kuchambua neno lenyewe limeshajichambua Mwenye Masikio na alisikie asiye na Masikio…………]
No comments:
Post a Comment