Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 3, 2023

MH KIKWETE NA KATIBU MWENEZI WATETA JAMBO MSIBANI


 

KUMBUKIZI.

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mh Jakaya Kikwete akitaniana na Katibu Mwenyezi wa CCM Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro. Selemani Kasanga.

Wanaoshuhudia tukio hilo kulia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro lnnocent Kalogerezi na kushoto ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare.

 Tukio hilo lilinaswa na Mwandishi wa Mtandao huu kwenye Msiba wa Mama Mzazi wa Mh Kalogerezi ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki.

Mh Kikwete anayejitoa sana kwenye Misiba ya watu wa kada zote alifunga safari kutoka Msoga Mkoa wa Pwani hadi Morogoro eneo la Mji Mpya kushiri Msiba huyo Mwanzo Mwisho.

Baada ya kuona wawili hao wanataniana Mwandishi wa Mtandao huu alitinga eneo hilo na kuwapiga Picha Viongozi haowakiendelea na utani wao Kasanga ni Mwanachama na shabiki lia lia wa Simba huku Mh Kikwete akiwa shabiki namba moja wa Yanga.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...