Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, July 5, 2023

MAKALA YA KUMBUKIZI YA HAYATI NYERERE NA HAYATI MANDELA


 

KUMBUKIZI.

Viongozi bora Afrika walioheshimiwa na Mataifa yote duniani ambao vifo vyao viliitikisa dunia.

Nao si wengine ni Rais wa awamu ya kwanza  Tanzania. Hayati Julius Kambarage Nyerere’Baba wa Taifa’ aliyefariki dunia Octobar 14 1999 Pichani[Kulia] na Rais  wa Kwanza Mwafrika wa Taifa la Afrika Kusini  Hayati Nelson Mandela aliyefariki dunia Desemba 6- 2013.

                      SIFA ZAO.

Maraisi hawa walikuwa Wazalendo wa kweli kwenye nchini zao na watu waliowaongoza. Hayati Mandela alikubari kutoa sehemu kubwa ya maisha yake kama sadaka ya kuwakomboa wa Afrika kusini, baada ya kufungwa jela kwa miaka 27 kwa sababu ya misimamo yake ya kisiasa dhidi ya Makaburu. Alivyoachiwa huru 1994 aligombea Urais wa taifa hilo kubwa Afrika na kufasnikiwa kushindi nafasi hiyo ya Urais.

Siku alipoapishwa alisema maneno hayo kwamba hatalipiza kisasa kwenye utawala wake na kwamba kwenye utawara wake atawaunganisha wa South Afrika kuwa wamoja.

 Kwa mshangao wawengi Mh Mandela alitawara kwa Mwaka mmoja kisha akang’atuka na kuwapisha wengine kutawala taifa hilo lenye nguvu kubwa kiiuchumia Afrika.

Halikadharika kwa Mpendwa wetu Mwl Nyerere alitukomboa watanzani 1961 akatuongoza kwa mafanikio akijenga umoja usawa na kuondoa ukabila na Udini akituunganisha tukawa kitu kimoja.

 Mwaka 1985 kwa ridhaa yale huku akiwa bado anapendwa na watanzania alitangaza kung’atuka madarakani akimuachia kijiti Rais Ally Hassan Mwinyi. Licha ya umaarufu wao na madaraka yao makubwa Wazee hawa hawakuwa mabepati wa kujilimbiukizia mali katika kuthibitisha hilo kwa sasa tunashuhudia familia zao zikiishi maisha ya kawaida kabisa.

 Pia walisaida saidia mataifa mengine ya Afrika kupata uhuru sambamba na kubeba jukumu la kusuruhisha migogoro kwenye mataifa mengi Duniani hasa bara la Afrika

 Binafsi nikibahatika kuingia Peponi kama sijawaona Marais hawa naweza kubeba ujasili wa kumuliza Mungu swali hilo kwa nini Nyerere na Mandela siwaoni Peponi?.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...