Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 8, 2023

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA MOROGORO AINGAMIZA TIMU YA MWAMNYETO FOUNDATION

                         Kikosi cha timu ya Moro Combine
                        Kikosi cha Mwamnyeto Foundation
Kipa wa Mwamnyeto Mohamed 'Nunda' ameacha gori wazi na kuamua kumfukuza winga wa Moro Combine lsmai Mgunda'Suma'
Show Show Winga hatari wa Moro Combine Jafar Salum Kibaya akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mwamnyeto Foundation
Kibaya Mkazi wa Changalawe Mzumbu anayekipiga timu ya lhefu 'Wana Mboga Maji wa Mbarali Mbeya akizidi kupiga mahesabu ya kumtoka beki huyo
Beki kagoma kafanikiwa kuchukua Mali kwa Kibaya na kusepa nayo
Katika gemu hiyo kivutikio kikubwa walikuwa ni wachezaji wawili wa timu hizo  ambao ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  anatajwa kuwa tajiri namba Morogoro Mkoani Morogoro aliyeitumikia timu ya Moro Combani na Mtangazaji Maarufu nchini wa kipindi cha Michezo cha Radio Clouds Fm Shaff Dauda aliyeitumikia timu ya Mwamnyeto Foundation.

 Pichani Mh Abood akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akisalimiana na wacheaji wa Moro Combine. lfahamike Abood pia ni mchezaji wa timu kabambe ya Moro Veterani,

 Baadae Mtandao huu utarusha Picha mbali mbali za Matukio ya Mh Abood akifanya yake uwanjani kwa muda wote wa dakika 50 alizocheza.

                                       Shaffi Daud
                Mkuu wa Mkoa akisalimiana na Dauda
Mgeni Rasm wa gemu hiyo ya kirafiki kati ya timu ya Mwamnyeto dhidi ya Moro Combine Mh Adam Kigoma Malima akiwa na wamiliki wa Taaisisi wa Mwamnyeto Foundation Bakari Nondo Mwanyeto[kulia Mwenyeji wa Tanga na Zawadi Mauyya kushoto Mwenyeji wa Kata ya Kigonda Maghorofani Mkoani Morogoro. wachezaji hao wote wanakipiga Yanga Mabingwa mara 29
Moro Combani wakiandika bao la kwanza lililofungw ana winga lsimail Mgunda Maarufu 'Suma' Mkazi Sultan Area Manispaa ya Morogoro, Suma anakipiga timu ya Tanzania Prisons ya Jijini Mbeya. Kabla ya kujiunga na Wajela jela hao, Suma aliwahi kuitumikia timu ya Burkinafaso ya Mkoani hapa kabla ya kutimkia Stend United 'Chama la Wana' ya Mkoani Shinyanga.
Winga wa Mwamnyeto  Foundation Offen Chikolla Mkazi wa Vibandani Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro anayekipiga Geita Gold alisawawisha bao hilom na kumuacha kipa wa Moro Combine Geofrey Mmassa akishuhudia kw amacho mpira huo ukitinga wavuni
Clotous Chama Mwamba wa Lusaka akiuchomoa mpira huo wavuni
Chama baada ya kuuchomo wavumia aliubailisha wa watoto waokota mipira 'Ballboys' akawapa huo wa zamnai na kuuchukua Mpira Mpya

Mwanmba wa Lusaka Zambia Clotous Chama[kulia] aliyeitumikia timu ya Mwamnyeto Foundation akimtoka beki wa timu ya Moro Combine Yohan Haule
Chama anayecheza soka la kulibwa Klabu ya Simba akizidi kutumia akili nyingi kumtoka beki Haule
.Beki huyo baada ya kuzidiwa mbinu kamua kumchapa mtama Chama ndani ya 18
Chama akiramba nyasi za uwanja wa Jamhuri kama alivyonaswa na kamera za kisasa za Mtandao huu zenye uwezo wa kupiga picha 6 tukio moja kwa sekunde 2
Kwangu mimi hiii ilikuwa Pelnaty zaili lakini Refa anayeonekna Pichani alitafsili hiyo sio Pelnaty
Baada ya kunyima Pelnaty Chama akimuangalia Mungu Wake juu mbinguni
...Chama akimtazama refa kwa jicho la husuda baada ya kumnyima pelnatym,refa ndio huyo anayeonekana miguu akitimua mbia
Offen Chikola Jamaa huyu ni wa Moto kweli kweli akimtoka kwa kasi ya ajabu beki Moro Combine Yohah Jonson Haule


Kinbwana Shomari ' Sekulu' Mluguru Og wa Kinole Wilaya ya ,Morogoro Vijijini akichonga Kona
....Akitafuta sehemu sahihi ya kuupeleka Mpira Picha zote na Dustan Shekidele,Morogoro., 

                Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 MCHEZO wa hisani wa kuchangia pesa za kusaidi watoto yatimu  uliopigwa jana uwanja wa Jamhuri Morogoro kati ya timu ya Mwamnyeto Founda dhidi ya timu ya Moro Combine, umetamatika kwa Katimu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro'MRFA' Mchungaji Emmanuel Kimbawara kuiangamiza timu ya Mwamnyeto kwa kufunga kiufnsiho Pelnaty ya sita. 

Katika gemu hiyo iliyojaza umati Mkubwa wawatu timu hizo zilitoka sale ya bao  1-1 hivyo ikaamuliwa iligwe mikwaju ya Pelnaty kwa lengo la kumpaya mshindi, timu zote  zilifanikiw akufunga Pelnaty zote tano ikaingia hatua ya piga ni kupige kwa maana ya penati moja moja. 

Mwamnyeto Foundation alianza kupiga Peltaty hiyo ya sita ambapo mkwaju makali wa Frank Chumvi alipangiliwa na Kipa wa Moro Combine Geofrey Mmassa, 

Katibu Mkuu Kimbawara alibeba jukumu la kupiga Pelnaty  ya Sita ambapo aliipa ushindi timu yake ambapo alifunga bao safi baada ya shuti lake kali kugonga mwamba wa juu na kujaa wavuni akimuacha kipa wa Nunda akigaragara bila mafanikio.
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...