. Nikiwa na Mwanafunzi wangu Neema D. Shekidele shule ya Sekondari. Kigurunyembe.
MARKO 8.1-10
”Katika siku zile kwa vile ulivyokuwa Mkuu tena ule Mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake akawaambia.
Nawahurumia mkutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami,wala hawana kitu cha kula.
Nami nikawaagiza waende zao nyumbani kwao hali wanafunga watazimia njiani na baadhi yao wametoka mbali.
Wanafunzi wake wakamjibu je ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani?.
Akawauliza mnayo mikate Mingapi?wakasema saba.
Akawaagiza Mkutano waketi chini,akaitwaa ile mikate saba, akashukuru akaimega akawapa wanafunzi wake wawandikie,wakawaandikia mkutano.
Walikuwa na Visamaki Vichache,akavibariki akasema waandikieni na hivyo pia.
Wakala, wakashiba wakakusanya mabaki ya Vipande vya Mikate makanda saba.
Na watu waliokula wapata elfu nne, akawaaga.
Mara akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake,akaenda pande za Dalmanutha.”
Hilo ndilo neno la Mungu jumapili ya leo Julai 23.
Ifahamike watu hao nne waliohesabiwa kula hiyo mikaye sana na wanaume pekee, wanawake na watoto hawakuhesabiwa ingawa walishiriki kwenye mkutano huo na kula Mikaye hiyo.
.
No comments:
Post a Comment