Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 24, 2023

JOTO LA TAMASHA LA SIMBA DAY LINAZIDI KUPANDA SHABIKI ALIYETOKA BUKOBA NA BAISKERI AFUNGUKA MAZITO.














 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

JOTO la Tamasha la Simba Day[Wenye hati miliki ya Matamasha hayo yanayoigwa na wengine] linazidi kupamba Moto, baada ya  Mwanachama wa timu hiyo Odax Alphonce Kaitasa[30] kutumia usafiri wa baiskeri kutoka nyumbani kwake Kijiji cha Kashozi Kitongoji cha Kashekulo, Kata ya Nyakato Wilaya ya Bukoba Mkoa wa Kagera kuelekea jijini Dar kwenye tamasha hilo. 

Shabiki huyo ametinga mkoani Morogoro juzi Julai 22 na kupokewa na wanachama na mashibiki wa tawi kuu la Simba, Maarufu tawi la Shujaa, ambapo viongozi wa tawi hilo walimpiga simu Mwandishi wa Mtandao huu na kumjulishua ugeni huo. 

Ndani ya dakika 0 Mwandishi huyo alitinga kwenye tawi hilo lililopo ndani  ya Jengo la CCM Kata ya Mji Mpya pembezoni mwa Soko kuu la Kata ya Mji Mpya na kumshuhuda ‘Mwamba’ huyo akizungukwa na mashabiki wa Simba waliojazana kwenye tawi hilo wakishuhudia tamasha la siku ya Mwananchi kupitia Luninga.

 Mwanahabari wa Mtandao huu anayeongoza kwa habari za chini ya kapeti mkoani hapa alimnyofoa Odax kutoka kwenye kundi hilo la wanasimba na kumsogeza sehemu tulivu na kufanya naye mahojiano maalumu.kama ifuatavyo.

Mwandishi. Mwamba  pole na safari.

Odax. Asante sana namshukuru Mungu nimefika Morogoro salama na kupokewa vizuri.

Mwandishi. Ok awari ya wote tungependa kujua histori fupi ya maisha yako, kwa maana umri wako, kazi yako na kama unafamilia kwa maana ya mke na watoto.

Odax. Nimezaliwa 1992.kazi yangu ni Mkulima pale kijijini, Sija oa na sina Mtoto ndio najitafuta kimaisha kwa sasa.

Mwandishi.Wewe ni shabiki tu wa Simba au ni shabiki Mwanachama mwenye kichinjio kwa maana ya kadi .

Odax. Ni Mwanachama hai wa Simba kutoka tawi kuu la Simba Bukoba.

Mwandishi. Wasomaji wa Mtandao wa Pendwa wa Shekidele wangependa kujua umetoka wapi na unaelekea wapi?

Odax. Nimetoka Bukoba kwa usafiri huu wa baiskeri naelekea Dar kwenye tamasha la chama langu  ‘Simba Day’.

Mwandishi. Umetoka Bukoba lini?

Odax Nimetoka Bukoba alfajiri ya tarehe 1-7-2023 hivyo nimetumia siku 22 kufika hapa Morogoro.

Mwandishi. Njiani hukupata matatizo yoyote kwa maana ya kuporwa na Vibaka kwenye misitu minene au kushambuliwa na wanyama nyakati za usiku sambamba na vizuiwi  ulivyovuka mipaka kutoka Wilaya moja kwenda nyingine?

Odax. Toka nimeanza safari sijasafiri usiku ikifika jioni na lala kwenye kijiji husika au Wilaya husika alfajiri naanza safari,hivyo sijaporwa wala kushambuliwa na wanyama wakali, kuhusu kuvuka kwenye mipaka ya Wialaya na Mikoa, nilipotoka Kijijini kwangu nilipewa kibari cha safari na Uongozi wa serikali ya Kijiji nilipofika Dodoma julai 13 pia nilipewa kibali na Jeshi na Polisi vibali vyote viwili hivi hapa.

Mwandishi. Kweli umejipanga hongera sana je kuna mtu amekufadhiri kwenye safari hii kwa maana ya chakula,Maradhi na Posho?

Odax, Hakuna mtu yoyote aliyenifadhiri nimejitolea mwenyewe kwa mapenzi yangu makubwa kwa timu yangu ya Simba, kipekee nawashukuru mashabiki na wanachama wenzangu wa simba  njiani ninapopita wananipa chakula, Maji, posho na sehemu ya kalala giza linapoingia, kana unavyoona wanasimba wa tawi hili la Morogoro wamenipokea na kunipa chakula na sehemu ya kulala.

Mwandishi.  Bukoba hadi Morogoro ni zaidi ya Kilometa 1.500 je huko njiani baiskeri haijakusumbua  kwa maana ya kuharibika sambamba na mipira kwisha kwa jua kali kwenye Lami?.

Odax. Swali zuri njiani nilipata pacha za kawaida niko fulu kwenye begi kuna spana na dawa za kuziba pacha na spana Malaya inayofungua sehemu mbali mbali, nilipofika Dodoma Mipira ya nje ilikuwa vipara sana baada ya kuliwa na Lami hivyo nilitafuta mingine sijabahatika kuipata,  kuna shabiki mmoja wa Simba kashauri tuiuze kwa bei ya chini tukafanya hivyo akaniongezea pesa tukanunua baiskeri mpya ambayo ndio hii.

Mwandishi. Utaondoka lini kuelekea Dar?

Odax. Baada ya kufika hapa Moro Viongozi wangu wa Bukoba wameniambia nisiwe na haraka ya kufika Dar wamenishauri nipunguze spidi ili nifike Dar tarehe 5 siku moja kabla ya tamasha, hivyo leo jumamosi ma kesho jumapili nitalala hapa Moro, jumatatu alfajiri Julai 24 nitaanza safari ya kuelekea Dar. Mwandishi. Je baada ya tamasha hilo la Simba Day lillopangwa kufanyika Julai 6 uwanja wa Mkapa Dar kutamatika utarejea Bukoba kwa baiskeri au utapanda basi?.

Odax. Haaa lengo lililokuw akufikishwa ujumbe kwa mapenzi yangu kwa timu hiyo hivyo baada ya tamasha nitareja Bukoba kwa basi.

 Mwandishi. Swali la mwisho ambalo ni lakizushi, kunawatu haswa mashabiki wa timu pinza hawaamini kama kweli umetoka Bukoba kwa baiskeri wanadai huko maporini unapakiza baiskeri yako kwenye malori ukifika kwenye vijiji umashuka na kuendelea na safari hao unawapa majibu gani?

Odax. Siku zote utopolo niwatu wa kupinga kila kita kama kuna mtu hamini basi jumatatu nikianza safari tuongozake yeye awe kwenye pikipiki au gari akae nyuma yangu aone ninavyofukuza lami, Nyerere Day watu walitoka Dar mpaka Butiama kwa baiskeri mbana hao utopolo hawakupinga kwa nini wapinge kwa mimi shabiki wa Simba

Mwandishi Ok Mwamba asante kwa time yako na safari njema.

Odax Asante sana wewe ni Mwandishi pekee kufanya mahojiano na mimi Asante pia naomba hizo picha ulizonipige chukua namba hii watumie viongozi wangu wa Simba kule Bukoba.

Mwandishi. sawa limekwisha hilo, labda neno la mwisho kwa wanasimba wenzio.

Odax. Nawashukuru sana wanasimba wenzangu wote walionipa msaada kwenye safari yangu, kupitia wewe mwandishi nawaomba Viongozi wangu wa Simba makao makuu wanipokee kijana wao tarehe 5 Mungu akipenda nafika makao makuu ya klabu yetu wanipokee.

Mwandishi Ok Mwamba  salamu zimefika

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...