Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, July 19, 2023

EXCLUSIVE ENTERVIEW. MCHEZAJI WA ZAMANI WA TAIFA STARS ASIMULIA ALIVYOPOFUKA MACHO.


Wachezaji wa zamani wa zamani waliocheza na Mzee shiwa walikutwa nyumbani hapo wakimfariji mwenzao.
Kulini ni Hemed Tindo aliyecheza na Mzee shiwa Mseto na kushoto ni Nassibu Waikera aliyecheza na Mzee shiwa timu ya Moproco.

                                     Mzee Shiwa Lyambiko
 

                           Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi.ama baada ya salam tuendelee na stori yetu iliyonza jana ya mchezaji wa zamani wa timu za Mseto, Tumbaku.Moproco na timu ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ Shiwa Lyambiko aliyepofuka macho. 
 
Baada ya jana kuelezea kwa kirefu Maisha yake ya Soka alipofanya mahojiano Maalumu na Mwandishi wa Mtandao huu nyumbani kwake kichangani mkoani Morogoro, leo tunamalizia simulizi hii kwa Mzee Lyambiko kusimuliza mkasa uliopelekea kupofuka macho wote mawili.
 
” Baada ya kuacha kucheza Mpira timu ya Kiwanda cha Moproco kufuatia kiwanda hicho cha mafuta ya kupikia kukumbwa na ukata timu ilivunjwa kwa bahati nzuri nilipata ajira kwenye Kiwanda hicho, zoezi la ubinafsisha wa Viwanda Utawara wa hayati Mkapa Kiwanda chetu kilibinafsihwa kwa Makampuni ya Abood. 
 
Baadae kindacha hicho kilifungwa baada ya kusitisha uzalishaji, hivyo Uongozi wa Abood ulinihamishia kiwanda kingine cha matulubai cha Canivas ambacho pia walibinafshiwa na serikali, nikiwa na cheo cha AfisaUtumishi na Utawara”alisema Mzee Shiwa na kuendelea kufunguka.
 
”Nakumbuka Mwaka 1994 natoka kazini Canivas majira ya saa 4 usiku nikiwa na usafiri wangu wa Pikipiki nilipofika jirani na kiwanda cha Ngozi upande wa pili kulikuwa na kichaka ghafra nikaona kitu kimenipanda mgongoni kikitokea kwenye kichaka.
Nikasimama na kujipekua sambamba na kufua shati lakini kitu hicho sijakiona nikawasha Pikipiki nikaendelea na safari ya kureja nyumbani Kichangani. 
 
Nilipofika nikamsimulia Mke wangu akanitia moyo akidai labda tawi la jani la mti limeniangukia, asubuhi nimelekea kazini nikiwa na afya njema siku hiyo kazi hazikuwa nyingi hivyo majira ya saa 11 nilitoka kazini nilipofika kwenye mzunguko wa barabara pale Msamvu jirani na Stend nilizungukwa na upepo 
 
mkali[Kivuravumbi]mchanga mwingi umeingia machoni.
Nikawasha Pikipiki nikaendelea nasafari ya kureja nyumbani nilipofika nikamsimulia tena mke wangu safari hii naye kaingia woga akanishauli nikaoge nilipooga bado hali ikawa tofauti macho yanawasha. 
 
Hali hiyo iliendelea kwa wiki nzima tukamua kwenda hospital mbali mbali ikiwemo KCMC Moshi bila mafanikiwa. 
 
Hali ilivyozidi kuwa mbaya baada ya uwezo wangu wa kuona kupungua kwa asilimi 70 niliandika barua ya kupunzika kazi, miezi miwili mbele machoyangu wote mawili yalikufa mpaka sasa sioni kabisa.
 
Yaani hawa tu washirikina wanatutesa sana”alimalizi akusema Mzee shiwa kwa sauti ya kinyonge. 
 
Alipoulizwa kwamba maisha ya binadamu Macho ndio dira hivyo kwa zaidi ya miaka 30 inaishi bila macho anamudu viti kuendesha maisha yake? Alijibu.
 
“ Naishi hivyo hivyo maisha ya tabu ingawa watoto zangu wakiongozwa na Msafiri Shiwa anayefanya kazi kwenye Mabasi ya Abood wananisaidia sina tena ujanja mimi ni wahapa hapa nyumbani tu”alisema Mzee Shiwa.
 
Kwa yoyote takayeguswa na tatizo lililomkuta Mzee wetu amfariji kwa kumpigia kwenye namba yake 0719 00 66 78.Hii ni mara ya tatu Mtandao huu unaripoti taarifa za wanasoka kukumbwa na matatizo ya Macho. 
 
Mara ya kwanza Mtandao huu uliripoti habari ya mcheza wa Hamis Ocheni aliyepofuka macho yote mawili baada ya kumbukwa na Upepo mkali kivurambi, katika hali ya kupigania kuokoa macho ya Ocheni Mwandishi wa Mtandao huu kwa kushirikia na Mchezaji
Shiza Kichuya wakiwashirikisha wadau wengine wa soka Mkoa wa Morogoro walianda mchezao wa kirafiki wa kuchangua matiabu ya Ocheni, ambaye hadi leo naye amepoteza uwezo wa kuona.
 
Mingine ni Kocha wa timu ya Burkinafaso Damian Maarufu Ticha Dame ambapo Mwandishi wa Mtandao huu kwa kushirikiana na aliyekuwa katibu Mkuu wa chama cha Soka Wilaya ya Morogoro Kafale Maharaganda walichangicha pesa kwa wadai na kufanikishwa matibabu wa Ticha huyo ambapo kwa Neema ya Mungu amepona na juzi nilikutana naye anaona vizuri tu.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...