Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, July 18, 2023

MCHEZAJI NYOTA WA ZAMANI WA MSETO NA TIMU YA TAIFA APOFUKA MACHO.


             Shiwa Lyambiko akihojia na Mtandao huu juzi


Na Dustan Shekidele,Morogoro. 
 
Hivi karibuni Mtandao huu ulipokea taarifa zikidai mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Mseto ya Morogoro na timu ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ Shiwa Lyambiko amepofuka Macho yote mawili. 
 
Kufuatia ukumbwa wa habari hiyo Mwandishi wa Mtandao huu alifunga safari hadi nyumbani kwa mchezaji huyo maeneo ya Kichangani Manispaa ya Morogoro na kufanya naye mahojiano Maalumu, huku akifunguka mazito jinsi alivyopata upofu huo. 
 
Awari kabla ya kuzungumzia upofu huu Mchezaji huyo alitakiwa kuelezea historia ya Maisha yake ya soka, ambapo alisema yeye alikuwa miongoni mwa wacheji walioshiriki katika kikosi cha Mseto kilichotwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Mwaka 1975.
 
”Nashukuru nimiongoni mwa wachezaji wa Mseto walioweka rekodi ya Kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza nje ya mkoa wa Dar es salaam kwa maana ya kuzipiku Simba na Yanga ”alisema Mzee Shiwa 
 
Alipotakiwa kikitaja kikosi hicho cha Mseto kilichotwaa ubingwa alifunguka haya.
 
”Nisiku nyingi zimepita lakini ngoja nijaribu kukitaja nitakao wasahau utanisamehe,
 
[1]Hamad Bongisa’Masarakasi’ ambaye nayeye kwa sasa unasumbuliwa na Macho.
 
[2]Abdan jina la pili nimelisahau
 
[3]Ramadhan Matola
.
[4]Miraj Salum,
 
 
[5]Matola Mkubwa.jina lake la kwanza nimelisahu mdogo wake ni huyo Ramadhan.
 
[6]Aluu Ally.
 
[7] Shiwa Lyambiko[Mimi mwenyewe niliwakimbiza sana]
 
[8]Hassan Shiringi
 
[9]na[10]nimewasahau
 
[11]Jafar Spensa.
 
Mfadhiri wetu alikuwa Karama[Mwarabu].
 
Baada ya kutwaa ubingwa tukapata tiketi ya kushiriki michuano ya Klabu bingwa Afrika tukakipiga na timu moja ya Uganda tukafungwa bao 7-0 na kutolewa kwenye michuano hiyo”alisema Mzee Lyambiko anayesifiwa kwa kupiga mashuti makali.
 
Mwaka huo huo wa 1975 Mzee Shiwa aiitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichoshiriki michuano ya Challenge Cup. 
 
“ Nakumbuka kwenye michuano hiyo ya Challenge tulicheza fainali na Kenya baada ya kutoka sale tukawafunga kwenye mikwaju ya Pelnaty 4-3 nakumbuka tuliofunga pelnaty hizo ni Jella Mtagwa.Ramadhan Mwinda.Mohamed Msomari na Mimi Shiwa Lyambiko. 
 
Alipotakiwa kutofautisha au kulinganisha wachezaji wa zamani na sasa Mzee Shiwa alisema.
 
”Wachezaji wa sasa licha ya kulipwa pesa nyingi lakini wengi wao uwezo wa kufunga mabao ni mdogo na sababu zinazopeleka kutofunga mabao wanataka kupiga mashuti gorini wakiingia kwenye 18 au kwenye 6,ambapo kiuhalisi maeneo hayo huwa na mabeki wengi hivyo hawawezi kukupanafasi ya kupiga shuti.
Sisi zamani hasa mimi na Victor Nkwanwa tulikuwa tukifunga mabao mengi kwa mashuti ya mbali tukiwa Free. 
 
Tukiwahada makipa wakihisi natoa pasi kumbe nafumua shuti, japo sioni lakini nasikiliza mpira kwenye redio huyu mtoto Mayele anafunga sana kwa sababu anapiga mashuti ya mbali ya kustukiza”alisema Mzee shiwa aliyewahi pia kuzitumikia timu za Tumbaku iliyomilikiwa na kiwanda wa Tumbaku Morogoro na timu ya Moproco iliyomilikiwa na kiwanda cha Mafuta ya Kula Morogoro. 
 
Simulizi hii itaendelea kesho kwa Mzee shiwa kusimulia alivyopata upofu akiwa njiani akitokea kazi kurejea nyumbani kwake, hivyo endelea kuwa jirani na mtandao huu muda wote.
 
Pichani Mzee shiwa akizungumza na Mwandishi wa habari hizi juzi.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...