Profesa Madundo Mtambo
Mkurugenzi Profesa Madundo Mtambo akizungumza kwenye Tamasha hilo lililofanyika Mei 27 kwenye Uwanja wa Shujaa uliopo Mji Mpya Manispaa ya Morogoro.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
TAASISI ya Moro Kids inayoongoza nchini kwa kuzalisha wachezaji wengi nyota wanaomba kwa sasa kwenye timu mbali ,mbali za ligi kuu zikiwemo timu kubwa za Simba, Yanga na Azam ljumaa ya June 16 yatafanya Maadhimisho kutimiza miaka 25 ya kuzaliwa kwa kituo hicho.
Akizungumza na Mtandao huu Mratibu Mkuu wa kituo hicho Rajabu Kindagule alisema tamasha hilo litafanyika katika Uwanja wa Sabasaba Mkoa hapa
Akifafanua Zaidi Mratibu huyo alisema”Maadhimisho hayo yataambatana na mechi mbalimbali ikiwemo ya Wachezaji wote waliopita hapa kituoni”alisema Mzee Kindagule ambaye ni Mwamuzi Mstaafu wa ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Mratibu huyo aliwataja baadhi ya wachezaji hao watakao shiriki tamasha hiyo kusapoti kituo chao kilichoibua vipaji vyao kuwa ni pamoja na Mzamiru Yassin,Hassan Kessy,Dickson Job,Shomari Kapombe,Kibwana Shomari,Nickson Kibabage,Abuutwarib Mshery,Hamad Waziri,
Wengine ni Offen Chikola,Ladack Chasambi,Frank Kahole,Shiza Kichuya,Johnson Clement,Paschal Msindo na Baraka Masenga.
lfahamike baada ya ligi kuu kutamatika June 9 wachezaji wengi watareja mapunziko majumbani mwao hivyo Taasisi hiyo imeamua kutumia mwanya huo kuwatumia wachezaji hao kwenye sherehe yao ambayo ilizinduliwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Shujaa kwa michezo mbali mbali ukiwemo wa Maaskofu na wachungaji wa KKKT Kukipiga na wenzao wa kanisa la Anglikana
Mbali na Mastaa hao kwenye tamasha hilo pia watu maarufu wamealikwa akiwemo Mkurugenzi wa Tan Warriors Sports Academy ya Dakawa Mvomero Mainga Ole Kataila na timu Kabambe ya Moro Veterani ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo ya Moro Kids Prof.Madundo Mtambo ni Miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment