Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, June 2, 2023

BODA BODA AFUNGUKA MAZITO KIFO CHA SHABIKI WA YANGA.


Big Suma akihojiwa na Mtandao huu kijiwe cha Boda boda, jengo kubwa linaloonekana mbele  Frem ya Kwanza ni Bucha ambalo Marehemu ‘Wille Yanga’ alikuwa akifanya kazi.

 Upande wa nyuma aliposimama Mpiga Picha wa Mtandao huu kuna Soko Kuu la Kata ya Mji Mpya.


 


                         Na Dustan Shekidele,Morogoro. 

Boda boda lsmail Shabani aliyempakia shabiki wa Yanga hayati William Hebes Maarufu ‘Wille Yanga’ametoa ushuhuda wa maneno ya mwisho aliyoambiwa na marehemu wakati akimpeleka stend ya Mabasi ya Msamvu. 

Akizungumza na Mtandao huu jana kwenye kijiwe  cha boda boda kilichopo Soko Kuu la Kata ya Mji Mpya, boda boda huyo Maarufu ‘Big Suma’ alisema amepata pigo kubwa kwa kifo cha shabiki  huyo ambaye kimsingi alikuwa mteja wake mkubwa anayempa kazi ya kusambaza nyama kwa wateja.

 “Shekidele mimi ni mdau mkubwa wa Mtandao wako kila siku lazima nisome habari zako Moto moto, juzi na jana uliposti vizuri  habari za kifo cha shabiki mwenzangu wa Yanga Mzee Wille.

Nimewiwa nikuite nikupe habari mpya za marehemu ambaye mimi ndio niliyembena ljumaa usiku  kumpeleka Msamvu ambapo alipanda gari na kuelekea Dar kuangalia gemu ya Yanga na USM Alger.

 Kweli siku ya kifo ikifika kinakuita, awari Yanga ilipotinga fainali kule South Afrika Wille aliweka nazili akidai  liwe jua au Mvua lazima siku ya fainali atinge Uwanja wa Mkapa kuweka histori ya kushuhudia Yanga ikicheza fainali ya CAF.”alisema Boda boda huyo mcha Mungu anayeswali swala 5.

 

Akiendelea kutoa ushuhuda boda boda huyo alisema. “ljumaa jioni Marehemu alimuaga bosi wake ambaye alimshauri asiende Dar kutokana na ugumu wa Maisha angalie Mpira hapa hapa Moro kupitia Tv aligoma akidai anataka kuweka histori kwenye maisha yake  kumbe anakifuata Kifo.

Kwa vile familia yake inaishi Chanika Dar  Wille aliingia Sokoni akanunua mchele kilo 10  akaingia buchani akakata  Paja la nyama nikambeba na mizigo yake nikampeleka Msamvu Stend akaenda zake Dar”alisema Boda boda huyo na kuongeza kudadavu.

“Jinsi alivyokuwa akiipenda Yanga hapa Morogoro anafamika kwa jina la Wille Yanga,jana nimeumia sana Marehemu Wille aliyeka Oda ya kununua gazeti la Jangwani kila linapotoka,  

 Muuza Magazeti  kama kawaida yake kamletea maremu gazeti hilo tukamwambia mteja wake amefariki dunia uwanja wa Mkapa, 

Muuza magazeti kachoka kamua kuvuta kiti kaketi kwa dakika kadhaa kisha kabeba magazeti yake kaondoka huku akiwa na simanzi zito”alimalizia kusema Big Suma ambaye anafanya  mazoezi ya kubeba vitu vizito na Mwandishi wa Mtandao huu kwenye Gym Pendwa ya Bad Boy iliyopo Ofisi Kuu ya CCM Kata ya Mji Mpya jirani kabisa na Soko.

              


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...