Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 4, 2023

ASKOFU PINDUA KAMA MAYELE.

                           Askofu Pindua akimiliki Mali
                          Akiambaa ambaa na Mpira
                                      .....Akiruka juu


                    ...Akipongezwa na Prof Madondo Mtambo
 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

ALIYEKUWA Makamo  Askofu  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania’KKKT’ Jimbo la Morogoro. Mch.George Pindua wiki iliyopita alikuwa kivutio kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Maaskofu na wachungaji wa KKKT dhidi ya wenzao wa Anglikana.

Gemu hiyo iliyotamatika kwa KKKT kuwachapa Anglikana bao 1-0 ilipigwa Mei 17 Uwanja wa Shujaa uliopo Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa.

Kwenye Mchezo huo kivutia kukubwa alikuwa Askofu Pindua aliyeingia dakika ya 62 ya kipindi cha Pili ‘Super Sub’ huyo mwenye Mwili Mkubwa baada ya kuingia alionyesha uwezo Mkubwa wa kumiliki Mpira kama Mkongomani Mayele’Mzee wa Kutetema.

 Baada ya gemu hiyo kutamatika Askofu huyo alimfuta Mwandishi wa Mtandao huu na kumwambia.

” Shekidele bado sijachoka nipige picha huku na ruka ruka hewani nikitetema kama Mayele”alisema Askofu huyo na kuangua kicheko.

Baadae Mmiliki wa Taasisi ya Moro Kids Profesa Madundo Mtambo ambaye ni kigogo serikali alimpongeza Askofu Pindua kwa uwezo wake wa Miliki Mpira.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...