Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, June 16, 2023

TANZIA . MWANAMUZIKI MAARUFU NCHINI AFARIKI DUNIA

                              Adolph Mbinga enzi za Uhai wake

 

 Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MPIGA Solo Maarufu nchini aliyetamba na Band  ya wazawa ya Afrikan Stars’Twanga Pepeta’ Adolph Nicholaus Mbinga amefariki dunia juzi kijijini kwao.

Taarifa zilizopatikana kwenye Group la Wanamuziki wa Tanzania zilieleza kwamba Mbinga amefariki dunia Alhamis Majira ya saa 5 usiku kijiji kwao Mpute Wilaya ya Nachingwea.

Mtoa taarifa alidai Mwanamuziki huyo alizidiwa na Ugonjwa ambapo siku chache kabla ya kifo chake aliacha kula hali iliyopelekea matatizo Zaidi kwa mpendwa wetu.

“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Tangulia Kamanda Pinga tutaonana baadae”.wote tuseme Amen

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...