Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, June 15, 2023

KUMBUKIZI. BAADA YA KUTWAA TUZO MSANII WA HIP HOP ATINGA KABURI LA MANGWEHA

Mwandishi wa Mtandao hu akiwa kwenye kaburi la Ngwea.

Mwandishi wa Mtandao huu akizungumza na Msanii Kala
Mama Mangwehe akiwa na Picha ya Marehemu Mtoto wake wakati akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi.
 

KUMBUKIZI

Msanii nyota wa Muziki wa  Hip hop Kala Jeremiah  mara baada ya kutwaa tuzo tatu  za Kilimanjaro Music Award mwaka 2013 kafunga  safari kutoka Dar Mpaka Moro kudhuru  kaburi la Msaani Mwenzake Marehemu Albet Mangweha’Ngweha’.

Mkali huyo wa Muziki huo wa kufoka foka alipotua Moro aliwasiliana na Mwandishi wa Mtandao huu ambapo wawili hao waliambatana mapka kwenye kaburi ka Ngweha

Baada ya kutoka kwenye kaburi hilo  lililopo nje ya Kanisa Katoriki Parokia ya Mtakatifu Monica Kihonda, wawili hao alitinga nyumbani kwa Mama Mzazi wa Hayati Mangweha ambapo Msanii huyo alimkabidhi  Tuzo Moja  Mama mzazi wa hayati Ngweha Bi Denisia Mangweha.

 Bi Mkubwa huyo  baada ya kupokea Tuzo hiyo aliangua kilio kwa uchungungu akimkumbuka Mpendwa Mtoto wake aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2013.

Mara baada ya kukamilika kwa makabidhiano hayo  yalifanyika nyumba kwa Mama huyo Mtaa wa Mazimbu Road Kihonda Mwandishi wa Mtandao huu alipata wasaha wa kuzungumza na Msanii huyo ambaye kwa sasa yuko kimya sana kimuziki.

 

    

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...