Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 26, 2023

PICHA MBALI ZA MASTAA WA LIGI KUU WAKIWEMO WA SIMBA, YANGA NA AZAM WALISHIRIKI TAMASHA LA MORO KIDS

Mgeni rasmi wa Tamasha la miaka 25 ya taasisi ya kuibua na kukuza vipaji nchini ya Moro Kids Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Tullo Fundi akisalimiana na mchezaji wa Morogoro All Stars Kiungo Punda Mzamiru Yassin ambaye pia ni mchezaji wa tegemo wa Simba.
Kiongozi huyo akisalimiana na mchezaji wa timu ya Moro Kids All Stars
Kikosi cha Mastaa wa Morogoro timu ya [Morogoro All Stars] Kipa ni Epimack Mwananziwa beki ya kulia Mkongwe Ally Shomari beki ya kushoto Mkongwe Jerry Santo beki ya kati walisimama Muddy Katoto na Kassim Ponela.no 6 kasimama Mzamiru Yassin no 7 Andrew Bundala no Ambrose Pamba [9 ]Jafal Kibaya[10]Edward Christopher na 11 Shiza Kichuya.
Kikosi cha Moro Kids All Stars kilichosheni wachezaji nyota wa ligi kuu Kipa ni kinda la Moro Kids Geofrey Mmassa anayejitafuta kwenye mafanikio ya soka.[2] Frank Kaole anayekipiga Mtibwa Sugar[3] Pascal Msindo anayekipiga Azam Fc[4] Nassir Kombo Maarufu Sccober[ anayekipiga Mtibwa Sugar[5] Jamal Masenga anayekipiga Tanzania Prissons[6] George Chota[Mtibwa Sugar[7] Jabil Saka[Mtibwa Sugar[8]Josepher Mkele[Mtibwa Sugar[9] Offen Francis[Geita Gold]10]Omary Sulatan[Mtibwa Sugar[11]Teps  Evance Azam Fc
Kiungo wa Morogoro All Stars Zawadi Mauya mwenye nguo nyeusi akiwa benchi, 

Mauya Mkazi wa Kihonda Maghorofani ni kiungo wa Mabingwa wa kihistoria Yanga

Beki kisiki wa Morogoro All Stars Shomari Kapombe' 'Shomi the way'[kati] akiwa bechi akifuatilia gemu kati ya timu yake iliyokipiga na Moro Kids All Stars. Kapombe Mkazi wa Mafiga Mkoani Morogoro aliingia dakika ya 75
Kiongozi wa shule ya Makongo ya jijini Dar Kanali Mstaafu ldd Kipingu akizungumza kwenye tamasha hilo la Moro Kids. lkumbukwe baadhi ya wachezaji wa moro kids baada ya kuhitimu eleimu ya msingi walipelekwa kwenye shule hiyo ya Makongo akiwemo Shiza Kichuya
Nyomi ya watu iliyofulika uwanja wa saba saba kuwashuhudia mastaa wa Moro Kids All Stars na wale wa Morogoro All Stars
Mzamiru Yassini Mkazi wa Kihonda Maghorofani akiwajibika kwenye gemu hiyo
Winga wa Moro Kids All Stars Teps Evance[kulia[anayeitumikia timu ya Azam akimtoka beki wa  Morogoro All Stars
Teps Mkazi wa Kilakala Morogoro akifumua shuti kali baada ya kumtoka beki wa Morogoro All Stars, hata hivyo shuti hilo halikuwa na macho lilitoka nje ya gori

Offen Francis akimtoka beki wa Morogoro All Stars, lfahamike Offen ni mchezaji tegemo wa timu ya ligi kuu ya Geita Gold

Offen  Mkazi wa Kiwanja wa Ndege akizidi kutimu mbio na kuwaacha mabeki wa Morogoro All Stars
Jabili Saka jezi no 7 akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao pekee kwenye mchezo huo, 

Mfungaji alifunga bao hilo akipokea pasi kutoka kwa Joseph Mkele jezi no 8. wachezaji wote hao waliohusika kwenye bao hilo wanakitumikia kikosi cha Mtibwa Sugar



Mmiliki wa kituo cha Moro Kids Profesa Madunso Mtambo akisalimiana na kijana wake Pascal Msindo aliyetoka kwenye kituo hicho na kujiungan na Azam Fc.

 Mzamiru Yassin kulia shiza Kichuya[kati] kushoto Jeery Santo.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...