Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 25, 2023

BYE BYE MBEYA CITY 2013-2023. USIYO YA JUA KUHUSU MBEYA CITY.




 

             Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Najua umesikia mengi kuhusu timu ya Mbeya City ‘Wana komakumwanya] a.k.a Wanyambara kushuka daraja jana kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa kumbukumbu ya Waziri Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine.

 

Wanyambara[Kwa kinyachusa ni Wanaume Mashujaa]jana hali imekuwa tofauti kwao baada ya  kuonyeshwa Unyambara na timu ya Mashujaa inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania’JWTZ’ Kikosi cha K.J 24 kilichopo  Kigoma’Mwisho wa Reli.’

 Mbeya City inayomilikiwa na Uongozi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya jana wameiga ligi kuu kwa vilio, baada ya kufungwa jumla ya bao 4-1 na timu ya daraja la kwanza ya Mashujaa,Kwenye mchezo wa Play Off.

lkumbukwe mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita Uwanja wa Like Tanganyika Kigoma, wenyeji Mashujaa waliichapa Mbeya City bao 3-1.

 

 Mchezo wa marejeano uliopigwa jana Uwanja wa Sokoine Mbeya Mashujaa tena wakaichapa Mbeya City bao 1-0 na kufanikiiwa kupanda dajara kutoka ligi daraja la kwanza kwenda ligi kuu kuchukua nafasi ya Mbeya City ambayo  wamekwenda ligi daraja la kwanza kuchukua nafasi ya Mashujaa.

USIO YA JUA KUHUSU MBEYA CITY.

Timu ya Mbeya City asili yake Morogoro, ambapo Miaka ya 2005 kuelekea 2009 Mkoa wa Morogoro ulikuwa na timu ya Rhino yenye Maskani yake Kata ya Kiwanja cha Ndege.

 Wakatui timu hiyo ikiwa daraja la Pili ilikumbwa na ukata mkali wa kiuchumi,hivyo katika hali ya kuinusuru isishuke daraja kwa kutofika kwenye vituo vya mchezo, Uongozi kwa kushirikiana na wanachama kwa kauli moja wameamua kuipiga mnada timu hiyo.

Nakumbuka  iliuzwa milioni 50 kwa  wachimba madini wa Mkoani Arusha, baade macharii hao wa migodini nao waliona timu hiyo kama ile mikopo ya kausha damu  wakaamua kuipiga bei kwa maafande wa JKT Oljoro Pia ya Arusha. 

Mwaka 2011 Madiwani wa jiji la Mbeya wakati huo wengi wao walitoka chama cha Chadema wakiongozwa na Meya wa jiji la Mbeya kutoka Chadema na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini kwa leseni ya Chadema Joseph Mbilinyi ‘Sugu’waliinunua timu hiyo kutoka kwa Oljoro.

Uongozi wa jiji ulipambana kuipandisha daraja timu hiyo nakumbuka mwaka 2012 ilipokuja hapa Morogoro kucheza na Burkinafaso kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza  baadhi ya madiwani wa Jiji la Mbeya wakijazana kwenye basi dogo aina ya Coaster wakiongozwa na Meya wao aliyekuwa kwenye Toyota V8 waliambatana na timu yao kwenye mchezo huo.

 Mwaka 2013 timu hiyo ilifanikiwa kupanda ligi kuu, baada ya kupanda waliibadili jina  kutoka Oljoro na kuibatiza jina jipya la Mbeya City.

Timu hiyo imedumu kwenye ligi kuu kwa miaka 10 mfurulizo ikipanda 2013 na kushuka 2023.

Kwa kheri  Mbeya City, kwa kheri wana Koma Kumwanya, Kwa kheri Wanyambara tukutane Champion Ship Septemba Mwaka huu.

Karibu Mashujaa Wetu Mliopambana na kuonyesha Ushujaa wenu kwa vitembo, baada ya mkoa wenu kukosa timu ya ligi kuu kwa miaka 20,baada ya Reli Kigoma iliyokuwa ikishiriki ligi Kuu kushuka daraja kwama 2003.

Mbeya City  kitu nitakacho Kimis kutoka kwenu ni ile Sytle yenu ya ushangiliaji mnapofunga bao.

 Mashujaa Mashujaa tukutane ligi kuu Agost Mwaka huu, Mayele na Yanga yake atakapokuja  kutetema huko Kigoma na Sako na Simba yake atakapokuja kuwanyunyizia ubani.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...