Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, June 27, 2023

MBILINGE MBILIGE ZA GEMU YA MASTAA WA SIMBA,YANGA NA AZAM

Shiza Kichuya akiitumikia timu ya Morogoro All Stars, dhidi ya Moro Kids All Stars, kwenye mchezo wa kirafiki wa kumbukizi ya Miaka 25 ya kuzaliwa kwa kituo cha kuibua na kukuza vipaji cha Moro Kids.

Gemu hiyo iliyopigwa wiki end iliyopita Uwanja wa Saba Saba  Manispaa ya Morogoro imetamatika kwa Mastaa wa Morogoro Morogoro All Stars kupokea kichapo cha bao 1-0 Picha zaidi fungua profaili la Mtandao huu




Kichuya uso kwa Uso na Kipa hata hivo nyota huyo wa Namungo alishindwa kufunga bao baada ya shuti lake kukwada na kipa chukukizi wa Moro Kidss Geofrey Mmassa, Mmassa hajatoka bado yuko kwenye kituo hicho cha Moro Kids
Beki wa zamani wa Simba na Yanga, Hassan Kessy 'Kidingile' ambaye kwa sasa anakipiga Dodoma Jiji huku tetesi zikidai msimu ujao atajiunga na Tabora United akidhibitiwa na beki wa Moro Kids All Stars.




Winga chipukizi wa Mtibwa Sugar aliyeitumikia timu ya Moro Kids All Stars  Joseph Mkele[jezi no 8] akimiliki mpira huku akichungwa na beki wa Morogoro All  Stars.

Winga wa Morogoro All Stars Jafar Kibaya[akijitwisha mpira kwa kichwa kwa lengo la kufunga bao huku Kipa wa Moro Kids All Stars Geofrey Mmassa akinyaka mpira huo na ukiweka salama timu yake,

 lkumbukwe Kibaya ni mchezaji wa lhefu ya Mkoani Mbeya



Beki wa Mtibwa Sugar aliyeitumikia timu iliyoibuka kipaji chake ya Moro Kids All Stars Nassir Kombo 'Scobber' wakimdhibiti winga wa Morogoro All Stars.


Scobber akimiliki Mpira Picha zote na Dustan Shekidele,Morogoro
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...