Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, June 1, 2023

MWANAMKE AKUTWA AMEFARIKI DUNIA GEST.

Mwenyekiti wa Mtaa huo akihojiwa na Mtandao huu nyumbani kwake juzi.

 


              Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Mwanamke mmoja’Mrembo’Helena Masanja anadaiwa kufariki dunia akiwa ndani ya nyumba ya Kulala Wageni’Gest’iliyopo Mtaa wa Makongoro  Mkoani hapa.

Tukio hilo limetokea Jumamosi ya Mei 28 ndani ya gest hiyo iliyopo eneo la Khahumba katikati ya Mji wa Morogoro.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo Mtandao huu Pendwa Duniani  lilitinga eneo la tukio na kufanikiiwa kuzungumza na baadhi ya mashuhuda ambao walikubali kuzungumza kwa sharti la kutotaja majina yao kutokata na mazingira ya eneo hilo ambalo ni maarufu kwa wadada poa kuuza miili yao.

” Jana tulikuwa tunafuatilia mechi ya Yanga na Waarabu baadae tunasikia huyu dada amefariki dunia ndani ya gest”walisema mashuhuda hao. 

Akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi nyumbani wake Mwenyekiti wa Mtaa huu Bi. Salah Saiti[Pichani mwenye dera za njano] alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye Mtaa wake.

” Mwenyekiti anaumwa mimi ni kaimu mwenyekiti,Siku ya tukio nilipokea taarifa za kifo hicho kutoka kwa muhudumu wa Gest akidai mteja wake amefia ndani.

Nilifika eneo la tukio na kushuhudia Mlango wa chumba  ukiwa umefungwa kwa nje huku kundi la watu wakimshuhudia marehemu kupitia Madirishani.

Nilitoa taarifa Polisi wakaja kuuchukua mwili kabla ya Polisi kufika marehemu alikuwa akiitwa majina mengi mengi hivyo Polisi walipofika na kupekua mabegi yake tukabahatika kupata kitambulisho chenye jina lake halisi la Hellena Masanja”alisema Mwenyekiti huyo.

Wakati tuna kwenda Mitamboni tulipokea taarifa zikidai  ndungu wa marehemu wametoka Mwanza kuja Morogoro kuchukua mwili wa Mpendwa wao na kwenda kupunzisha kwenye nyumba yake ya milele Mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro  Alex Mkama akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi kwa njia za simu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

               


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...