Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Jana Mtandao huu ulikuwa wa kwanza kuripoti eneo la biashara ya Shabiki wa Yanga hayati William Mhwani Hebes[60]na kuahadi leo kuingia mzigo kuchimba zaidi habari za chini ya kapeti za shabiki huyo.
Kwenye chimba chimba hiyo Mwandishi wa habari hizi amebaini Marehemu alikuwa akiishi mikoa 3 kwa wakati mmoja, Mikoa hiyo ni Dar es salaam inapoishi familia yake, Morogoro eneo lake la kazi na Dodoma mkoa aliozaliwa.
Asubuhi na mapema Mwandishi wa habari hii wakati akijiandaa kuingia mtaa kuchimba habari hiyo, alipokea taarifa nyingine ya kifo cha mwanamke mmoja kudaiwa kufariki dunia akiwa gest eneo la Khahumba.
Hivyo Mtandao huu uliamua kuanza na tukio hilo la moto moto, baada ya kutinga eneo la tukio na kukusanya habari hiyo sambamba na picha za tukio hilo mbazo zitaruka hewani hivi Punde.
Baada ya kukamilisha habari hiyo Mtandao huu unaojikita kwenye habari za chini ya kapeti alitinga soko la Mji Mpya na kuendelea na habari ya kifo cha Mwanachama huyo wa Yanga.
Baada ya kutinga kwa mara nyingine kwenye Bucha hilo lililopo eneo la Soko Kuu la Kaya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro.
Akihojiwa kwa njia ya simu Mmiliki wa Bucha hilo Bw William Telya alisema.
” Wajina wangu marehemu William Mhwani Hebes tunatoka kijijini kimoja cha Mvumi Dodoma nirafiki yangu wa siku nyingi aliamua kutoka Dar kuja Morogoro kufanya kazi kwenye Bucha langu huku familiya yake ikisalia jijini Dar.
Jumamosi majira ya usiku baada ya kufunga Bucha aliniaga akidai ana kwenda Dar kuangalia fainali ya timu yake ya Yanga iliyocheza na USM Alger.
Mara baada ya mchezo huo kutamatika tulipokea taarifa za kifo cha rafiki yangu aliyeaga dunia kwenye vulugu ya kugombea kuingia uwanja wa Mkapa”.alisema bosi huyo.
Alipoulizwa Marehemu atazikwa lini na mkoa gani alijibu.
” Kwa sasa msiba bado uko nyumbani kwake Dar kesho asubuhi wataanza safari ya kuelekea Dodoma kumpunzisha kwenye nyumba yake ya milele, nimewasiliana nao nitawasubiri pale Msamvu tunaungana kwenda Dodoma”alisema Telya.
Kwa Upande wake Kijana Mkapa Joseph aliyekuwa akifanya kazi muda wote na Marehemu William alipohojiwa muda mchache uliopita ndani ya Bucha hilo alisema
” Jumamosi majira ya saa 2 usiku Mzee William aliniambia kwa vile hajapata tiketi ya kuingia uwanjani ameamua kwenda Msamvu usiku huo kudandia gari lolote akalale Dar ili jumapili asubuhi adamkie Uwanja wa Mkapa kusaka tiketi usiku bosi ananipigia simu akidai Mzee Wille amefariki dunia uwanjani.
Yaani kwa siku mbili hizi hapa Buchani naona maluwe luwe niko peke yangu Mzee wangu ameondaka Aisee ”alisema Mkapa na kutokwa na machozi kama anavyoonekana Pichani
“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Tangulia Mwananchi uliyeifia timu yako tutaonana badae “ Wote tuseme Amen.
No comments:
Post a Comment