Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, May 3, 2023

UPENDO WA KWELI, SPIKA Dr TULIA AMFARIJI MJANE WA PROF MBIA.
















 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Tulia Ackson Jumapili iliyopita ametinga nyumbani kwa familia ya Prof Emmanuel Mbiya  na kumfariji Mjane wa Marehemu Bi Matha Mbia aliyefiwa na Mpendwa Mume wake hayati Prof Mbia.

 

Mara baada ya kuwasili nyumbani hapo maeneo ya Nane nane mkoani hapa majira ya mchana Spika Dr Tulia alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Anthony Mtaka ambaye ni miongoni mwafamilia hiyo.

lfahamike Mh Mtaka aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Mvomero Morogoro, Mkuu wa mkoa wa Simiyu. na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameoa mtoto wa kwanza wa familia hiyo aitwaye Neema Emmanuel Mbia Pichani  mwenye gauni lenye rangi nyeusi nyeusi.

 

Mara baada ya Mh Tulia  kutoa pole kwa familia hiyo, Mh Mtaka kwaniaba ya familia ya Prof Mbia alimkabidhi Kitabu Maalumu Spika huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini.

 

 Hayati Profesa Mbia hadi umauti unamfika alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine’SUA’ akimilikia pia Hotel Maarufu ya Gronency iliyopo Nane nane kando kando ya barabara kuu ya Moro-Dar. 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Tangulia kamanda tutaonana baadae.                        

                               CAPTION

Mh Dr Tulia  akiwasili Nyumbani kwa hayati Prof Mbia na kupokewa na Mh Mtaka. Picha no 2 Mh Tulia akimpa mkono wa Pole Mjane wa Marehemu.

Picha no 3 Mh Tulia akisaini kitabu cha Maombolezo huku Mjane wa Marehemu na watoto zake 3 wakishuhudia tukio hilo

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...