Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, May 24, 2023

RUVU SHOOTING YAPATA KIGUGUMIA KUTANGAZA UWANJA WATAKAO UTUMIA LIGI DARAJA KWA KWANZA.


                               Kikosi cha Ruvu Shoooting


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Baada ya kushuka daraja Uongozi wa timu ya Ruvu Shooting inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa [JKT] Mkoa wa Pwani.wamepata kigugumiza kutaja uwanja watakaoutumia kwenye michuano ya Champion Ship msimu ujao.

 Jana usiku Afisa habari wa timu hiyo iliyokuwa inautumia uwanja wa Jamhuri Morogoro kwenye michuano ya Ligi kuu, Masau Bwire alikuwa akihojiwa na Radio Moja kubwa nchini kuhusiana na timu hiyo kushuka daraja.

Kwenye mahojiano hayo yaliyosikilizwa A-Z na Mwandishi wa Mtandao huu Afisa habari huyo alimuliza maswali mengi ya Msingi ambayo Masau Bwire aliyajibu vizuri.

Kama kawaida  Mwandishi wa habari hizi hua anaendeleza  pale walipoishia wengine, hivyo kwenye mahojiano hayo Masau Bwire hakuulizwa swali la uwanja watakaoutumia kwenye michuano hiyo ya ligi daraja la kwanza msimu ujao.

 Timu hiyo imekuwa ikihama viwanja mara kwa mara ilishawahi kucheza kwenye uwanja wao wa Mabatini Mlandizi baada ya uwanja huo kufungiwa na TFF kwa kukosa vigezo wakahamia uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Wakati ligi  ikielekea ukingoni Ruvu waliupa kisogo uwanja wa Uhuru, wakahamia Uwanja wa Jamhuri Morogoro, waliutumia mpaka wanashuka daraja.

Kwa faida ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro walioanza kujenga mahaba na timu  hiyo, mara baada ya mahojiano hayo jana usiku Mwandishi wa habari hizi alimtwangia simu Masau Bwire,baada ya kumpa pole za kwa timu yake kushuka daraja moja kwa moja Mwandishi huyo alikwenda kwenye swali lake la msingi la  uwanja watakoutumia  msimu ujao.

”Hooo Shekidele swari zuri naomba nipe muda bado tuko kwenye vikao, tutautangazia uma uwanja tutakaoutumia kwenye michuano yetu ya ligi daraja la kwanza msimu ujao”alisema Masau Bwire kwa sauti ya upole.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...