Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, May 29, 2023

MAPYA YAIBUKA SHABIKI ALIYEFARIKI DUNIA JANA UWANJA WA MKAPA DAR.


 Bucha ambalo marehemu Wille alikuwa akifanya biashara ya nyama ya Ng'ombe

              Na Dustan Shekidele,Morogoro.

lmebaini yule shabiki aliyefariki dunia jana kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika Kati ya wenyeji Yanga na USM Alger, aliyefamika kwa jina moja la William alikuwa Mfanyabiashara kwenye bucha hili la nyama lililopo maeneo ya Mji Mpya Mkoani hapa.

Baada ya kupokea taarifa hizo jioni ya leo Mwandishi wa habari hizi alitinga kwenye bucha hilo lililopo eneo la Soka kuu la Kata ya Mji Mpya na kushuhudia Bucha hilo likiwa limefungwa.

Kufutia hali hiyo Mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo aliyejitambusha kwa jina la Mama Rama.

” Ni kweli Shekidele Wille alikweda kucheki gemu ya Yanga jana na kwenye msukumano ule yeye pekee ndiye aliyefariki dunia bucha alilokuwa akiuza nyama lile pale limefungwa”alisema Mama Rama ambaye ni Mwanachama wa Simba kupitia tawi kuu la Shujaa lililopo eneo hilo la soko.

Kesho panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mtandao huu utaingia mzigoni kuendelea na uchunguzi wa habari hii iliyogusa watu wengi nchini hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...