Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, May 29, 2023

LICHA YA KUCHEZESHA MAMRUKI, WACHUNGAJI ANGLIKANA WAPOKEA KICHAPO DHIDI YA WACHUNGAJI WA KKKT.

Kikosi Kabambe cha Maaskofu na Wachungaji wa KKKT
           Kikoci cha Maaskofu na Wachungaji wa Anglikana
Beki kikosiki wa KKKT Thomas Poul Mkuu wa Jimbo la Morogoro na Mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Majengo Kihonda, Kabla ya kuhamisha Majengo Mch Poul alikuwa Mchungaji wa KKKT Usharika wa Mji Mpya ambao Mwandishi wa habari hizi ndipo anaposali.toka dasara la Watoto  'Sundar School'akapata Kipa lmara hapo hapo mpaka sasa anasali hapo. 

Kanisa hilo ndio hilo linalooneka pembesoni mwa uwanja huo wa Shujaa

Shughuri yoyote ya watumishi inaanza na kumaliza na Maombi kabla ya mchezo kuanza waliangusha maombi mazito uwanjani
Winga wa timu ya Anglikana Vedasto  Vahaye[kushoto mwenye jezi nyeusi] akimtoka beki KKKT, Thomas Poul.ambaye ni Mkuu wa Jimbo la Morogoro na Mchungaji kiongozi wa KKKT Usharika wa Majengo Kihonda Vedasto ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa Kuu la Anglikana lililopo Manzese jirani na Mzunguko wa barabara wa SUA.

Mchungaji Poul akimiliki Mpira huku Mchungaji Vedasto akimnyemelea
Mch Poul akitoa pasi kwa Kisigino huku akizongwa na Mamruki Mussa Miraj
...Cheki Mussa Miraji ambaye ni Meneja wa taasisi ya Moro Kids akinyemelea mpira unaomilikiwa na Mch Poul
Kipa wa KKKT Joseph Tengeneza akinyaka Mpira huku akilindwa na beki wakeSteven Banzi[kati] huku winga wa Anglikana Erick Chibada wa Anglikana akinyemelea mpira huo. 

Kipa Tengeneza ni Mwinjilisti wa KKKT Usharika wa Sokoine Dakawa Mvomero. Banzi ni Mchungaji wa KKKT Usharika wa Mkambarani huku Chibada ni mchungaji wa Anglikana kanisa la Chamwino.


Show Show Mchungaji Kibanda wa Anglikana akimchapa Mtama Mchungaji Banzi wa KKKT
Mchungaji Banzi yuko Makini kakwepa Mtama huo akiendelea na safari zake huku akimuacha nyuma mchungaji Chibada akishangaa

 Winga wa Anglikana Mchungaji Vedasto akimwaga maji kama waziri wa Maji baada ya kumtoka beki wa KKKT  Abuwe Myombo ambaye ni Mwinjilisti wa kanisa kuu la KKKT Usharika wa Bungo akihudumu Mtaa wa Mgeta. 

Awari Myombo alikuwa Mwanakwaya wa Kwaya ya Paradiso Usharika wa Mji Mpya kabla ya kujiongeza kwenda kusomea Uinjilisti

 


    Na Dustan Shekidele,Morogoro.

LICHA ya timu ya Wachungaji kutoka Makanisa yote ya Anglikana Jimbo la Morogoro kuchezesha Mamruki,imepokea Kichapo cha bao 1-0 dhidi ya timu Kabambe ya Wachungaji wa Kanisa la Kiinjiri la Kilutheri Tanzania’KKKT’Jimbo la Morogoro.

 Juzi Jumamosi ilikuwa ni siku ya Umoja wa Makanisa Tanzania’C.C.T Day’ na siku hiyo hiyo Kituo Maarufu nchi cha kukuza na kuibua Vipaji vya Soka cha Moro Youth na Moro Kids likifanya sherehe ya kumbukizi ya  Miaka 25 ya kituo hicho kinachoongoza nchini kwa kutoa wachezaji wengi wanaongara timu kubwa za Simba, Yanga, Azam na timu ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’.

 Kufuatia matukio hayo Viongozi wa Taasisi hizo za Moro Kids na CCT waliamua kuungana kwenye matukio hayo kwa kuandaa mchezo wa kirafiki kati ya Watumishi wa Mungu Maaskofu,Wachungaji na Wanjilisti kutoka KKKT na wenzao kutoka kanisa la  Anglikana Jimbo la Morogoro.

 

Katika gemu hiyo ilipigwa Uwanja wa Shujaa Majira ya saa 4 asubuhi  kipindi cha Pili Anglikana waliamua kuingiza Mamruki kwa lengo la kusaka ushindi.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo dakika 56 Anglikana walimuingiza Mamruki wa kwanza George Pindua Mchungaji wa KKKT na dakika 67 walimwingiza Mamruki mwingine Mussa Miraji ambaye ni Meneja wa Kituo cha Moro Kids ambaye pia ni Muumini wa dini ya Kiislamu.

 

Licha ya kuingiza Mamruki hao kwa lengo la kusaka ushidi Mungu alikuwa upande wa KKKT ambapo dakika 90 Mshambuliaji hatari wa KKKT Thomas Leban Moreti aliifungia timu yake ya KKKT bao hilo Pekee na kupeleke kilio kwa mashabi wa Angiliaka.

 

 lfahamike mfungaji wa bao pekee ni Mchungaji wa kiongozi wa Usharika wa Yeliko Wami Dakawa.

Baadae mtandao huu utarusha Picha za Askofu Pekee aliyekuwepo kwenye mchezo huo akimiliki mpira kama Mayele, hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...