Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, May 21, 2023

MAADHIMISHO YA UHURU WA HABARI 2023 YAFANA MOROGORO.

Maandamano hayo yakikatiza stend ya zamani ya daladala
                                ....Yakiwa eneo la Lunna
                          ....Yakikatiza Soko la Kingalu
              ...Yakikatiza jengo la PPF Mkoa wa Morogoroo
              ...Yakikatiza ofisi ya Manispaa ya Morogoro
                           ....Yakiktiza Mnara wa Posta
....Moja ya usafiri unaobeba waandishi wa habari  wa Tv lmaan ukiwa ukumbi wa Savoy
.....Maandamano hayo yakiwasili hotel ya Savoy iliyopo barabara ya stesheni
Mwenyekiti wa MOROPC Nickson Mkilanya wapili kutoka kushoto wakipokea maandamani hayo kwa kushirikiana na Waandfishi wa kongwe Samwel Msuya wa kwanza Kulia ambaye kwa sasa ni Mh Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Bujaga lzengo Kadago, Abed Dogori ambaye pia ni Meneja wa Abood Media na wa mwisho kulia ni Aziz Msuya Mwenyekiti Mstaafu wa MOROPC

Katibu Mkuu wa MOROPC Lilian Lucas Kasenene akizungumza baada ya washriki kuwasili ukumbini
Kaimu mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro'MSJ' Sir Erick akisalimia baada ya kutambulishwa, 

lfahamike asilimi 90 ya Waandishi wa habari mkoa wa morogoro tumesoma kwenye chuo hicho


Mwenyekiti Mkilanya akisoma hotuba yake kwenye Maadhimisho hayo

Watu weweeeeee.

Waandfishi wa habari Wakongwe nchini Amina said[kulia] aliyeahi kuzitumikia ITV na Radio One pamoja na Star Tv na Radio Free Afrika akilisakata Twisti na Mkongwe mwenzake Aziz Msuya aliye wahi kuwa meneja wa magazeti ya Mwancnhi Mkoa wa Morogoro


 


     Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Waandishi wa habari mkoa wa Morogoro jana wameandamana wakiadhimisha siku yao ya Uhuru wa habari dunia 2023.

 Maandamano hayo yaliongozwa na Jeshi la Polisi yakisindikizwa na band ya Matalumbeta, yalianzia Jengo la Shani Snema yakaelekeza stend ya zamani ya daladala yakaibukia Soko kuu la Mkoa wa Morogoro maarufu Soko la Chief Kingalu yakazunguka mzunguko wa barabara ya SUA yakelekea ukumbi wa Savoy.

 Maandamano hayo yaliyoshirikisha Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali vya Uandishi wa habari Mkoa wa Morogoro,Waandishi wa habari kutoka Vyombo mbali mbali  akiwemo Mwandishi wa Mtandao huu, yalipokelewa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya[ Mwenyeshati jeupe wanaopiga makofi].

Mara baada ya kupokea Maandamano hayo washiriki waliingia ndani ya Ukumbi na kujadilia mambo mbali mbali kuhusiana na Tasnia hiyo ya habari, miongoni mwa watu waliozungumza ni Mtangazaji Mkongwe wa Radio Tanzania[RTD] Kwa sasa Shirika la Utangazaji Tanzania[TBC] Bujaga lzengo Kadago a.k.a Baba Askofu tukio hilo litaruka hewani hivi punde.

Kitaifa Maadhimisho hayo yalifanyika May 3 Zanzibar na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ally Mwinyi.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...