Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, May 22, 2023

MAADHIMISHO YA UHURU WA HABARI DUNIANI,MWANDISHI MKONGWE AFUNGUKA MAZITO.

Bujanga lzengo Kadago akimwaga madini kwa Vijana wake

 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Waandishi wa habari mkoa wa Morogoro juzi wameadhimisha siku ya Uhuru wa habari 2023 kimkoa kwa Mtangazaji mkongwe nchini Bujanga lzengo Kadaga’Baba Askofu’ kufunguka mazito.

 Akizungumza kwenye Maadhimisho hayo ndani ya Ukumbi wa Savoy Mzee Bujaga ambaye kwa sasa ni Mstaafu alisema.

 

 “Licha ya kufanya kazi Redio Tanzania najivunia kuanzisha vituo kadhaa ya Tv na Redio Mwaka 1996 Mimi kwa kushirikiana na Waandishi wenzangu Betty Chalamila’Maarufu Betty Mkwassa na hayati Karim Besta tulianzisha  Dar.es salaam Televishen’DTV’ iliyomilikiwa na Mfanyabiashara Murtheza Dewji”alisema  Bujana na kuendelea kufunguka.

 Baadae mimi na hayati Besta tulikuja Morogoro kuanzisha Televishen ya Abood’ATV’ nikiwa Abood kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro liliniomba nikaisimamie redio Ukweli inayomilikiwa na kanisa hilo.

 

 Nikatoka redio ukweli nikajiunga na SUA Media nilipofanya kazi mpaka nilipostaafu kwa sasa niko nyumbani  Kasanga nikijishungulisha na Ufugaji wa Kuku”alisema Bujanga.

   HISTORIA FUPI YA MZEE BUJAGA.

Aliwahi kutangaza kwa mafanikio Radio Tanzania’RTD’sasa TBC Taifa akatoka huko akajiunga na ITV.Radio One.

Katika hali ya kusaka mkate wake akahamia Morogoro, Abood Media,akaachana na Abood akajiunga na  Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro’MSJ’ ambapo alimfundisha pia Mwandishi wa habari hizi kwenye chuo hizo wakati huo  madasara ya chuo hicho yalikuwa Ghorofa la CCM Mkoa.

 

 Mtafutaji huo akatoka kwenye chuo hicho akatimkia Radio Ukweli baada ya kuhangaika sana kwenye sekta binafsi Mzee Bujanga aliamua kurejea serikalini akijiunga na SUA Media inayomilikiwa na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine’SUA’ alipohudumu mpaka alipostaafu kwa mujibu wa sheria

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...