Na Dustan Shekidele,Morogoro.
FURAHA YA USHINDI.
Baada ya Mnyama Simba kumrarua Mwananchi kwa makucha mawili juzi kwenye Hifadhi ya kumbukumbu ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamini Wiliam Mkapa a.k.a ‘Lupaso’ Mara baada ya gemu hiyo iliyoanza saa 11 jioni na kutamatika saa 1 usiku kutamatika.
Mashabiki wa Simba walifunga Muziki Mnene’Kigodoro’ Kwenye Ki Bajaj waliozunguka Mitaa mbali mbali na kuishia tawi kuu la Simba Maarufu tawi la Shujaa lililopo Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro.
Walipofika kwenye tawi hilo lundo la mashabiki walichomoka kwenye Ki Bajaj hicho kama siafu na kuungana na Lundo la mashabiki waliokuwa kwenye tawi hilo kwa pamoja mashabiki hao wakimwaga Mauona na kupuliza Mavuvuzera wakifurahia kumfunga mtani wao huku waki watupia maneno ya shombo mashabiki wa Yanga waliokuwa wakiishi jirani na tawi hilo.
Mara baada ya Mwamuzi wag emu hiyo Mwana Mama Jonisi Nkya kutoka Kagera kupuliza kipenga cha mwisho Mwandishi wa habari hizi akiwa na Pikipiki yake ya Mwendo kasi aliingia mtaani kusaka matukio.
Matukio mengine yataruka baadae likiwemo la shabiki wa Yanga na tukio la mtoto shabiki wa Yanga kumgomea mama yake ambaye ni shabiki wa Simba.Hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote
No comments:
Post a Comment