Hayati Sokoine enzi za uhai wake.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
LEO April 12-2023 ni Kumbukizi ya miaka 39 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Edward Molinge Sokoine aliyefariki dunia kwa ajari ya gari hapa Mkoani Morogoro.
CHANZO CHA AJARI HIYO.
April 12-1984 Mpendwa wetu Mtumishi Mwadilifu wa wananchi Kiboko cha Wahujumu Uchumi Edward Molinge Sokoine akitokea Dodoma kuelekea Dar es salaam msafara wake ulipofika Dakawa umbari wa takribani kilometa 25 kutoka Morogoro mjini.
Gari aina ya Land Cruiser iliyokuwa ikitokea upande wa Morogoro iliyokuwa ikiendeshwa na Dumison Dube raia wa Afrika Kusini inadaiwa kuvamia msafara huo na kugongana uso kwa uso na gari ambalo alipanda kipenzi cha Watanzani Waziri Mkuu Sokoine.
Baada ya ajari hiyo Waziri Mkuu Sokoine alikimbizwa hospital ya Mkoa wa Morogoro ambapo alipatiwa huduma ya kwanza kabla ya kuhamishiwa hospital ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam ambako alifariki dunia wakati jopo la madaktari likiendelea kuupigania uhai wake.
Aliyekuwa rais wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarahe Nyerere aliutangazia Uma juu ya Kifo hicho cha mtetezi huyo wawanyonge.
“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lako lihimidiwe” .
“ Watanzania tutakukumbuka daima Mwendo umeumaliza tangulia Kamanda tutaonana baadae”
No comments:
Post a Comment